loader
Dstv Habarileo  Mobile
Sensa 2022 kisasa zaidi

Sensa 2022 kisasa zaidi

MKURUGEZI Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Dk. Albina Chuwa amesema sense ya watu na makazi itakayofanyika Agosti mwaka 2022 itakuwa ya kipekee tangu nchi ilipopata Uhuru mwaka 1961.

Chuwa ameyasema hayo leo mjini Dodoma katika uzinduzi wa Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yenye kauli mbiu ‘Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa’

 “Tofauti ya kwanza, sensa zilizopita tulitumia teknolojia ya makaratasi kwa asilimia 95, sensa ya nne ya mwaka 2012 tulitumia teknolojia ya ‘scanning’ sensa ya nne ilitupa matokeo ndani ya miezi mitatu. Sensa ya mwaka kesho Agosti itatupa matokeo ndani ya mwezi mmoja.

“Sensa  zilizopita tulikuwa tunatumia madodoso ya aina mbili, moja lenye maswali 64 kwa sensa ya mwaka 2012 na lingine fupi lilikuwa na maswali 20,” amesema.

Amesema katika uchambuzi wa sensa zilizopita, uchambuzi uliishia katika ngazi ya wilaya, watakwimu hawakuweza kwenda ngazi ya kata, kijiji na kitongoji.

“Ngazi ya kata, kijiji na kitongoji tulikuwa tunatoa idadi ya watu peke yake kwa sababu tulikuwa tunatumia teknolojia ya sampuli, asilimia 30, 40 kwa sensa zilizopita.

“Tofauti kubwa sana na sensa zilizopita, Serikali inaenda kufanya mazoezi matatu makubwa ya kitaifa, tunaenda kuhesabu watu kwa kuchukua taarifa zao za kiumri, kijinsi, uraia, elimu na shughuli zote wanazofanya sambamba na makazi yao, hilo ni zoezi tosha tunaita ‘traditional census’ kama ilivyoainishwa kwenye mapendekezo ya Umoja wa Mataifa.

“Katika sensa ya mwaka 2022 tunaenda kuongeza taarifa za majengo yote nchi nzima, vijijini na mijini. Tutaenda kukusanya aina ya paa, kuta, shughuli ndani ya majengo hayo… kama ni ghorofa sita makarani watapita jengo hadi jengo kupata wamiliki wote kwa nchi nzima. Hilo ni zoezi tosha,” amesema.

Amesema zoezi lingine kubwa ni kuchukua anuani za makazi katika majengo yote ya nchi nzima kwa maeneo ya mijini na vijijini.

“Tunaenda kuchukua anuani ya kila jengo, barabara au mitaa inayozunguka majengo. Lengo ni kufahamika ipasavyo makazi yako wapi na tunaenda kuchukua taarifa zote na kuweka kwenye kanzi data ya taifa, ukibonyeza taap! pale Kariakoo unajua kuna duka la nani na lipo sehemu na unaweza kufuatilia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0b0a25c646be287b6bf56e97b0ff51a8.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi