loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ujenzi wa Ikulu Dom wafikia  75%

Ujenzi wa Ikulu Dom wafikia 75%

MAENDELEO ya ujenzi wa  Ikulu  Chamwino jijini Dodoma umefikia asilimia 75 huku mkataba wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kisasa ukisainiwa.

Hayo yamesemwa leo na Rais Samia Suluhu, leo katika uzinduzi wa Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

“Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wa ikulu mpya na sasa umefikia asilimia 75.” amesema na kuongeza

“Ujenzi wa kiwanja kikubwa cha ndege cha kimaitaifa utaanza hivi karibuni kwani jana mkataba wa ujenzi huo umesainiwa.

Aidha alisema  ujenzi wa majengo mji wa kiserikali kule Mtumba unaendelea na kwamba  kutajengwa majengo makubwa ya ghorofa kutegemea na pesa ambazo kila wizara itapewa.

Amesama  tayari serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya mzunguko ambayo ujenzi wake ulicheleweshwa kwa sababu ya taratibu za fidia lakini sasa muda si mrefu utaanza

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/23e699fd938ecff47465f33e93b8d79d.JPG

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi