loader
Dstv Habarileo  Mobile
 Ibrahimovic kuikosa Liverpool

 Ibrahimovic kuikosa Liverpool

Mkali wa mabao wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic atakosa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.

Zlatan alirejea Jumapili iliyopita katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lazio, baada ya kukaa nje kwa takribani miezi minne akiuguza majeraha yake.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Man United, Barcelona, Juventus, Inter Milan na PSG, atalazimika kukaa nje katika mchezo huo baada ya taarifa kuwa alianza kuhisi maumivu akiwa mazoezini leo.

 Ibrahimovic ambaye mwezi ujao anatimiza miaka 40 alisaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuweka klabuni hapo hadi msimu wa 2021/2022.

AC Milan kesho itakuwa katika Uwanja wa Anfiled nchini England kukipiga na Liverpool katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6dd6ec466afbffc30226e43d0e1a3a1a.jpg

Ligi Kuu England leo inaendelea katika viwanja tofauti, ...

foto
Mwandishi: MILAN, Italia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi