loader
Dstv Habarileo  Mobile
Usaliti mchwa unautafuna vyama vya siasa

Usaliti mchwa unautafuna vyama vya siasa

WANASIASA na baadhi ya vyama vya siasa nchini haviwezi kushika dola kutokana na dhambi ya usaliti wanayoifanya kwa wanachama wenzao na kwa wananchi ambao ni walipakodi na waliowaamini na kuwapa uongozi.

Wakati wakudai Uhuru kulikuwa na utitiri wa vyama vya siasa vilivyokuwa na ushawishi mkubwa na kuungwa na wafuasi wao na viongozi hao hawajawahi kuwaangusha wafuasi wao wakijikita zaidi kwenye ajenda yakudai uhuru na kuwa Taifa huru.

Mpambano katika uwanja wa vita ya kudai uhuru ulikuwa mkubwa sana Barani Afrika hususani pale Ghana ilipojipatia Uhuru wak, kitendo ambacho kiliwasha moto wa vuguvugu lakudai Uhuru kwa mataifa mengine Afrika na moto huo huo Mwaasisi wa Taifa la Ghana Kwame Nkuruma aliitangazia Afrika kuwa Ghana haiwezi kuwa huru kama nchi nyingine hazina Uhuru.

Kauli hiyo ikaungwa mkono na Baba wa Taifa la Tanzania Mw Julius Kambarage Nyerere, Keneth Kaunda-Zambia, Robert Mugabe -Zimbabwe, Samora Machel-Msumbiji na mataifa yote barani Afrika kuungana na lao likawa moja na kuachana na historia ya vyama vyao, siasa zao, tofauti zao matokeo nchi zote Afrika zilipata Uhuru japo kwa njia tofauti lakini lao lilikuwa moja.

Mwaka 1992 mfumo wa Vyama vingi vya Siasa tukashuhudia (NCCR_Mageuzi ya Agustine MREMA ikianzishwa na vinginevyo kama, CUF ya akina James Mapalala, CHADEMA ya akina Edwin Mtei na Bob Makani pia vyama vingine kamavile, TLP, TADEA, UPDP, CHAUSTA, UDP, CHAUMA, na ACT_WAZALENDO) vyama hivi vilikwenda vizuri kabisa bila shida yoyote.

Lakini kinachoendelea sasa ni tofauti na madhumuni yakuanzishwa vyama vingi kwa mantiki hiyo hatunabudi kufanya tathimini kwa vyama vyetu ambavyo ndivyo vinaifanya siasa ya nchi kuwa siasa bora au bora siasa lakini mwisho wa siku tunategemea vyama hivyo vishike dola na kuongoza nchi hivyo basi ipo hoja yakuwatathimini kama wanatosha au laa..

Tathimini za kitafiti na kitaalamu ni muhimu kwa majira haya ili kujua Kisiasa wapi tumetoka, wapi tulipo na Tunakwenda wapi katika kufanya mapinduzi makubwa ya "siasa za kizalendo"

Kwasababu Siasa zetu ndio msingi mkubwa wa Kukua Kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni ambapo  mjumuisho wa yote hayo Tangu Enzi za Nyerere tunapaswa kujifunza na kubadilika kwa Mustakabali wa maisha yetu na kuachana na siasa za kimaslahi badala yakujitoa kwa wanachi.

Mwanafalsafa wa kijamii kutoka Amerika ya kaskazini mwaka 2000, aliandika kitabu chake cha {"Declaration of Independence"} nanukuu anasema> " Politics is pointless if it does not hing to enhance the beauty of our lives" mwisho wa kunukuu.  ' Yaani siasa itakuwa si kitu ikiwa haitapendezesha maisha yetu.

Nayasema haya kwakuwa nafuatilaia siasa za Tanzania na ulimwenguni nikiangalia mwenendo na uendeshaji wa vyama vyetu vya siasa asilimia 90 ya vyama vyetu haiendani na maudhui ama malengo yakuanzishwa kwake na vingi vimekuwa vijiwe vya upigaji fedha.

Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa ilikuwa ikihakiki uhai wa vyama vya Siasa nchini ambako kumeibuka madudu mengi ndipo unapojiuliza. Je wanasiasa hawa wanaongoza vyama hivi wanaelewa wanachokifanaya au wanajitoa ufahamu? Na je wananchama wao wanaelewa wanakoelekea au wanapiga maktaimu?

Ziara ya Msajili Msaidizi Sixity Nyahoza ilipofika ofisi za Chama cha SAU ilibaini kuwa chama hicho hakina hata akaunti ya Benki, wala vitabu vya risiti ambazo wananchama wao walipaswa kupatiwa lakini fedha za michango zinapaswa kuhifadhiwa benki na hata kama kuna wahisani wapitishie benki.

Msajili msaidizi anatoa maagizo kwa uongozi wa SAU kufungua akaunti benki nakuuagiza uongozi kutoa risiti kwa kila shilingi inayochangwa na kila aina ya manunuzi swali la kujiuliza hapa je? Uongozi wa chama hiki kweli una malengo yakushika dola nakuwatumikia wananchi? na je wanachama wa chama hiki wanajielewa? na je hizi kumbukumbu alizooneshwa Msajili msaidizi ni za kweli kuwa wana wanachama hai?

"Tuwe makini kwenye masuala mapana na nyeti, kushika dola na kuongoza nchi si jambo dogo, kuwepo kwa utitiri wa vyama vya siasa nchini siyo kukuwa kwa demokrasia bali hudhoofisha demokrasia wakati mwingine”

"Nitawapeni mfano mmoja wa chama fulani katika jimbo la Temeke Dar es Salaam kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020 nikiwa nimeketi mahali kwenye ukumbi fulani ambao una baa pia niliona kundi la wakina mama wengi ambao nawafahamu na robo tatu yao ni waumini wa vyama vitatu vikubwa vya siasa nchini wakishiriki katika mchakato wakumdhamini mgombea urais wa chama hicho jina kapuni"

Nilimhoji mmoja wao nikamuuliza mbona kule... nakuona, huku nako upo, alichonijibu ni kwamba "hapa mjini ishi kwa akili kile chama kikubwa tuna kadi za kudumu na zina maana yake tupo ambao ni vindandakindaki tupo ambao hatutaki fursa zitupite unataka mkopo wa vikundi na asilimia kumi za halmashauri bila kuwa huko utazitoa wapi? " huku nako tumefuata fursa ya mda mfupi kama hapa tumekula tumekunywa na elfu ishirini tumembulia siku yakupiga kura akili kumkichwa'Nikawa hoi na hapa ndipo tulipofikia siasa za ubangaizaji.

Badala ya kuyaishi malengo ya kuanzishwa kwa vyama hivyo badala yake vimekuwa vitegauchumi, chama hakina akaunti hata rudhuku ya serikali kikibahatika kupata itapitia wapi ni mambo ya ajabu vyama hivi havinabudi kubadirika.

Kama vikundi vya kijamii vina akaunti chama cha siasa kinachotaka kutuongoza hakina akaunti je hapa kuna chama au upatu ni lazima wananchi tutafakari tutalia kila siku kuwa chama tawala kinaiba kura au NEC inakibeba chama fulani kumbe ni mifumo mibovu ya vyama.

Abdallah Chaulembo Mjumbe wa Chama cha Wananchi CUF tawi la Buguruni anasema "Mwandishi siasa uzisikie tu kuna figisufigissu sana kwenye siasa na mizengwe isiyoisha ndiyo maana wanachama hujiongeza nakuangalia upepo kweli wengi wana kadi zaidi ya moja na mwisho wa siku vyama huangukia pua kwenye matokeo.

Ziara ya Msajili inatua Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) nako inakukuta kamfumo kama kale ka SAU japo kana tofautiana kidogo hapa anakutana na ukiukwaji wa utunzaji wa kumbukumbu za mali za chama ambapo chama hicho kikuu cha upinzani nchini hakizingatii uwekaji wa kumbukumbu za mali za chama hicho kama kanuni za fedha za usajili zinavyotaka.

Hakina orodha ya mali, bajeti wanayotumia haidhinishwi na kamati kuu lakini ikumbukwe hiki ni miongoni mwa vyama vinavyopata ruzuku kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wawakilishi bungeni lakini hawana orodha je ni kwa manufaa ya nani? na je wanachama wanalijua hili na je wanachama wanaumiliki wowote kama sehemu ya mhimili wa chama hicho ndiyo maana nasema nina mashaka nawanachama wetu kama wanajua nafasi zao katika vyama vya siasa.

Chadema wanashindwa hata kuweka picha ya Rais katika ofisi zao je ni kwamba hawamtambui rais Samia Suluhu Hassan? au kwakuwa anatokana na chama cha mapinduzi ? kwahiyo wanasubiri watakaposhika dola waweke picha ya raisi wao? na kama ni hivyo watawezaje kuongoza na kusimamia rasilimali za nchi kama rasilimali zao tu taarifa zake ni siri kwa msajili na kwa wanachama wanaowaongoza?

Kadhalika kuwa na taarifa za Manunuzi ya chama tena kwa manufaa yao lakini wao hawana je huku siyo kuwatega wanachama? ingawa chama hiki kinapongezwa kwa mfumo mzuri wa kidijitali kwa ajili ya kanzidata za wanachama wao.

Ukiacha la chadema ukirudi nyumba kubwa Chama cha Mapinduzi ikilinganishwa madhumini yakuanzishwa kwake na kinachoendelea sasa kuna dosari ndogondogo ukilinganisha na mafanikio makubwa waliyonayo CCM.

Suala la mamluki ni mchwa ambao unakitesa chama hiki, siku hizi kumekuwa na tabia ya umamluki ambapo Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo alishaonya hili katika vikao vya ndani ya chama na hata hadharani kupitia vyombo vya habari.

Hata hivyo vyama vya siasa nchini vinalaumiwa kutoka katika misingi ya kitaasisi na kuwa mali za watu binafsi yaani viongozi huvifanya vyama kama mali ya kifamilia na siyo taasisi hili ni jinamizi linalotesa taifa.

"Naitwa John Rutashoborwa ukitaka kujua kuwa siasa imekuwa kweli mchezo mchafu katika harakati za kupigania chama tunakuwa pamoja lakini katika fursa kama za uongozi kuanzia shina hadi taifa, udiwani na ubunge hapo ndiyo utaona majina ya watoto wa waasisi wa vyama husika wakijitokeza nakuwania nafasi za juu na wanapata je hivi ni vyama vya kifamilia au?

TANU hawakufuata haya yanayofanyika sasa hivi walizingatia utaifa na majimbo kuwa kila mkoa au wakati majimbo yote yatoe wawakilishi wanaotoka eneo husika  lakini siku  hizi hatuna vyama vya siasa ni pata shika" anasema Rutashoborwa.

Makala hii inavitaka vyama vya siasa kurejea kwenye mstari na kujenga imani kwa wanachama na watanzania kwa ujumla ili kulilitea Taifa maendeleo kwakutanguliza uzalendo kwanza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e0cb15356658ac1c21f4d21677cc0afe.jpg

MAZAO mengi ya chakula, matunda na biashara kama ...

foto
Mwandishi: Dunstan Mhilu 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi