loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bilioni 17.9 kujenga chuo cha ufundi Nala

Bilioni 17.9 kujenga chuo cha ufundi Nala

SERIKALI imetoa kiasi cha Sh bilioni 17.9  kwa jili ya ujenzi wa Chuo kikubwa cha Ufundi Stadi (VETA) kinachojengwa eneo la Nala mjini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu mjini Dodoma leo ambapo alisema Ujenzi huo utakamilika hivi karibuni na chuo kitaanza na udahili wa wanafunzi 1500 lakini baadae watafikia 5000.

Aidha kwa upande wa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema kukamilika kwa chuo hicho kutaleta manufaa katika kuzalisha vijana wenye ujuzi ambao watakwenda kutumika katika viwanda mbalimbali vinavyoendelea kujengwa.

“Ujenzi huu ulianza June mwaka huu na unatarajiwa kumalizika Disemba 2022, ujenzi unaendela vizuri, nchi inakwenda katika viwanda hivyo tumepanga kuzalisha wataalamu wengi katika vyuo hivi” alisema Kipanga.

Awali Mhandisi Msaidizi kutoka Kampuni ya BICO, Aliki Nziku, amesema mradi huo ni mpango wa Serikali kuongeza Wataalam katika nyanja za ufundi  na Teknolojia.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo alitembelea na kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari mfano iliyopo Iyumbu inayojengwa na SUMAJKT kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 17 ambayo inatarajiwa kuanza kuchukua wanafunzi January 2022

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3cab9aed48ccd2b496ac417ce3239c74.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi