loader
Dstv Habarileo  Mobile
Halmashauri zashauriwa kuwasaidia waathirika wa madawa kiuchumi

Halmashauri zashauriwa kuwasaidia waathirika wa madawa kiuchumi

HALMASHAURI zimeshauriwa kuwasaidia walioathirika kiuchumi na uraibu wa madawa ya kulevya ambao wameacha tabia hiyo, kwa kuwapa mitaji kupitia mpango wa utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Luteni Josephine Mwambashi alitoa ushauri huo wakati Mwenge ulipotembelea kituo cha matibabu kwa watu walioathirika na dawa za kulevya kilichopo katika Hospitali ya Kanda ya N yanda za juu kusini ilyopo Mbeya.

Luteni Mwambashi aliyasema hayo kufuatia watu wanaopata huduma kituoni hapo kutoa ushuhuda wa mabadliko chanya tangu walipoanza kupata matibabu lakini wakasema changamoto kubwa baada ya kubadili mienendo na tabia zao ni kurejea katika maisha ya mtaani ambayo ndiyo awali yaliwaingiza kwenye matumizi ya dawa hizo.

Awali akitoa taarifa ya kituo hicho,Daktari bingwa wa afya ya akili, Dk Beatrice Thadei alisema hadi sasa wanufaika wa kituo hicho wamefikia 394 kati yao 378 ni wanaume na wanawake ni 16 tangu Julai 2017 wakati kliniki hiyo ilipofunguliwa.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/55a55c032b7a1f9b12aab264c22e0b28.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Na Joachim Nyambo,Mbeya.

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi