loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mradi wa Maji Bunda, Butiama kaa la moto, Aweso ashusha nyundo

Mradi wa Maji Bunda, Butiama kaa la moto, Aweso ashusha nyundo

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso, ameelekeza kuondolewa wahandisi wawili wanaosimamia Uratibu wa Miradi ya Mugango-Kiabakari Butiama na Ujenzi wa Chujio la Maji Bunda baada ya kushindwa kutimiza majukumu yao.

Aweso ametoa maelekezo hayo leo Septemba 14, 2021 katika ziara yake wilayani Butiama, Bunda na Musoma vijijini.

Waliondolewa ni Mratibu mhandisi Maria Bwire (Mugango-Kiabakari-Butiama) na Mhandisi Nicholaus Angumbwike (Mradi wa Chujio la Maji Bunda).

Aweso alidai kuwa wahandisi hao wameshindwa kufuatilia ipasavyo utekelezaji wa miradi na uratibu na pia kutokuwepo uwandani (site) wakati wa ziara yake.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f514bbeff34ce4fee3a061722c7f966f.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi