loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mongela apiga mkwara ‘vizabizabina’, Atangaza Neema kwa wamachinga

Mongela apiga mkwara ‘vizabizabina’, Atangaza Neema kwa wamachinga

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kwa kushirikiana na viongozi wa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu ‘Machinga’ wanatazama mfumo wa kuwapanga ili waweze kufanya biashara zao vizuri.

Mongella ameyasema hayo leo Septemba 14,2021  akizungumzia  maagizo aliyoyatoa Rais Samia Suluhu, kwa wakuu wa mikoa kuwapanga upya wamachinga katika maeneo yao bila kutumia nguvu na vurugu ili walipe kodi na kufanya biashara zao vema

Alisema Mkoa huo umejipanga kwa ndani yani kushirikisha watu husika na kamati ya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutazama mifumo ya upangaji wafanyabiashara kwa kushirikisha viongozi wa machinga

Mongela alisema hakuna hakuna anayewachukia machinga na asitokee mtu mmoja kujifanya anawapenda sana machinga na wala asitokee mtu yoyote anayejifanya anawachukia sana.

“Hakuna mtu yoyote anayechukia na Rais Samia Suluhu amelionyesha hilo waziwazi kutowachukia wafanyabiashara,” alisema Mongela

 Alisema bahati mbaya suala la machinga katika baadhi ya  maeneo linatumika kama siasa na kupotosha dhana halisi ya kujitafutia maisha na kuwasihi  machinga waiamini serikali yao na wamwamini Rais Samia kwani rais ni mtu anayejali haki za binadamu na anayejali utu wa mtu

Alitoa rai asitokee mtu yoyote anayedhani anaweza akavuruga maelekezo hayo ya Rais  kwani  atadhibitiwa,

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d4a080e0e327d9da9d3c410a12ec6096.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi