loader
Dstv Habarileo  Mobile
TRA yavuka lengo la makusanyo Rukwa

TRA yavuka lengo la makusanyo Rukwa

MAMLAKA ya Mapato ya Tanzania (TRA) Mkoa wa Rukwa imekusanya zaidi ya Sh bilioni 19.7, ikiwa ni asilimia 128 ya lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa TRA Mkoa wa Rukwa, Fredrick Kanyilili wakati wa semina ya wafanyabishara wa Manispaa ya Sumbawanga juu ya mabadiliko ya sheria na kanuni za kodi ili wazifanyie kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti, alifungua semina hiyo huku akisisitiza wafanyabishara wote waone aibu kukwepa kulipa kodi.

Kanyilili alieleza kuwa, lengo lilikuwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 15.5.

"Nina furaha kuwatangazia kuwa hadi Juni 30  mwaka huu, TRA Mkoa wa Rukwa ilikusanya Sh 19,709,923.49  na kuvuka lengo likiwa 15,393,550,000 kwa asilimia 128,"alieleza.

Akifafanua alieleza kuwa, mafanikio hayo ni kutokana na uhiari wa wafanyabishara kulipa kodi, elimu kwa mlipakodi iliendelea kutolewa pia matumizi sahihi ya mashine za EFD's. 

Mkirikiti aliwataka wananchi kulipa kodi kwa wakati kwa mujibu wa sheria zitakazosaidia serikali kuimarisha uchumi wake na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aliitaka mamlaka hiyo kuendelea kuunga mkono mikakati ya serikali kwa kuwaeleza wananchi umuhimu wa kulipa kodi.

"Hivi itasaidia kuchochea maendeleo ya taifa. Itawezekana kwa walipakodi kuzingatia ulipaji wa kodi," alisisitiza.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo, aliwataka walipa kodi kutembelea ofisi za mamlaka hiyo kupata maelekezo muhimu.

Pia aliwataka wananchi kuhakikisha wanapewe stakabadhi ya bidhaa walizonunua kutoka kwa wafanyabishara.

Baadhi ya wafanyabishara waliohudhuria semina hiyo waliiomba mamlaka hiyo kutafsiri nyaraka na machapisho kwa lugha ya Kiswahili ili iwe rahisi kwa kuzielewa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3d7876e1c1ec7838eeed6185ff3a5635.png

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi