loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bil 314/- zatengwa miradi ya maji Pwani

Bil 314/- zatengwa miradi ya maji Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amesema jumla ya Sh bilioni 314 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mkoani humo ili kuondoa adha kwa wananchi. 

Kunenge alibainisha hayo katika ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada  ya kutembelea mradi wa maji katika Kijiji  cha Mwanambaya Kata ya Mipeko wilayani Mkuranga. 

Alisema mpaka sasa tayari  Dawasa na Ruwasa wameshatekeleza miradi ya upatikanaji wa maji na kuwafikia wananchi kwa wastani wa asilimia 78.

"Mpaka  sasa taasisi hizi Dawasa na Ruwasa zinaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji kwa asilimia 78 katika maeneo tofauti, hivyo  changamoto ya huduma ya maji itapungua,"alisema. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno, amewaomba wananchi kutunza miundombinu ya maji na  kulipa gharama za uendeshaji kwa wakati ili pindi inapotokea matengenezo ya miundombinu yafanyike kwa haraka.

"Miradi hii ni chachu ya maendeleo kwa hivyo wananchi hatuna budi kulinda miundombinu hii ya maji na kuwa na utaratibu wa kulipa ankara za maji kwa wakati, "alisema Maneno.

Akisoma taarifa Kaimu Meneja wa Maji Ruwasa, Maria Malale, alisema mradi wa maji  katika Kijiji cha Mwanambaya ulianza kutekelezwa Julai 2018 na miundombinu ya mradi huo inatarajiwa kusambazwa kwa umbali wa Kilometa 39 na  gharama zilizotumika ni Sh bilioni 2.3.

Malale alisema mradi huu unakadiriwa kuhudumia kaya 800 na mpaka sasa maombi ya kaya yaliyopokelewa kwa ajili ya kuunganishiwa maji ni 71 kati ya hizo tayari kaya 21 zimeshaunganishwa na zinatumia huduma hiyo.

Diwani wa Kata ya Mipeko, Adili Kinyenga,  alisema kuna wananchi wanaunganishiwa maji kwa gharama kubwa hivyo amewaomba watumishi wa Dawasa kurudi ofisi za kijiji na kata na kujadili namna ya kuziendea gharama hizo bila kuathiri watumiaji wa huduma ya maji.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d0985a7a99dbff84d06ed5d3922fe3ca.jpeg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Sophia Malaki, TUDARCo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi