loader
Dstv Habarileo  Mobile
Solskjaer amtetea Lingard ‘naye binadamu’

Solskjaer amtetea Lingard ‘naye binadamu’

“Jesse Lingard atajifunza kutokana na makosa yaliyowapa faida timu ya Young Boys ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchster United,” amesema Ole Gunnar Solskjaer kocha wa United.

Kauli hiyo imekuja baada ya jana Manchester United kuambulia kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu hiyo, baada ya Lingard kutoa pasi kimakosa iliyowapa ushindi wapinzani wao.

United ilicheza pungufu kuanzia mwishoni mwa kipindi cha kwanza, baada ya beki wao Aaron Wan Bissaka kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Christopher Martins.katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pasi mbovu ya Lingard ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo iliwapa ushindi wapinzani wao baada ya Jordan Siebatcheu kufunga bao la pili la ushindi.

“Sisi ni binadamu, kila mchezaji anafanya makosa,”alisema Solskjaer.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d481f0ba2d9bb5889e4752e8f69f6ca5.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: BERN, Switzerland

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi