loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia: Tanzania inafuata msingi ya demokrasia

Rais Samia: Tanzania inafuata msingi ya demokrasia

Rais Samia Suluhu amesema kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa kufuata misingi ya demokrasia.

Akizungumza leo katika Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam, Rais Samia alisema Tanzania misingi ya kijamaa, isiyokuwa na dini na yenye kufuata mfumo mwa vyama vingi.

“Hakuna shaka kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongozwa kwa kufuata misingi ya Demokrasia, katiba inatamka wazi kuwa ni nchi ya kijamaa isiyokuwa na dini yenye kufuata msingi wa vyama vingi,”alisema Rais Samia.

Alisema Serikali imechukuwa hatua mbalimbali katika kuanzisha, kusimamia na kuimarisha misingi na taratibu za taasisi zinazosimamia masuala ya demokrasia.

Aidha, Rais Samia alikiri kuzifahamu changamoto za demokrasia zilizopo nchini na kwamba changamoto hiyo ipo mpaka kwenye mataifa mengine duniani kote.

Bado zipo nchini, na hii ni kwa sababu hakuna taifa duniani ambalo linaukamilifu katika masuala ya demokrasia, demokrasia pamoja na ukweli kwamba ni lengo au shabaha lakini pia ni mchakato ni suala endelevu"alisema Rais Samia.

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi