loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dk Sengati ataka taarifa za watumishi wasio waadilifu

Dk Sengati ataka taarifa za watumishi wasio waadilifu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati amemuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kishapu, Emanuel Johnson kuwasilisha kwake taarifa ya kina ya wafanyakazi wake ambao kwa kiasi kikubwa wanasababisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kishapu kutotekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa.

‘’Nakupa jukumu ili Mkurugenzi kutuletea taarifa ya kina ya wale wote ambao unaamini ndio wanasababisha kusuasua kwa miradi ya ujenzi wa Maabara na Zahanati awe Mkuu wa Idara au mtumishi lakini pia na sisi tutachunguza kupitia vyanzo vyetu ili tuweze kuchukua hatua ya kina kubaini nani anahusika katika kushindwa kutekeleza miradi katika kiwango kinachotakiwa Dk Sengati

Dk Sengati amefikia hatua hiyo baada ya kutembelea mradi wa ukarabati wa vyumba vya maabara katika Shule ya Sekondari Ukenyenge pamoja na mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mwaweja vilivyopo Wilaya ya Kishapu na kujionea namna ambavyo ujenzi wa miradi hiyo ulivyo chini ya kiwango.

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Emanuel Johnson alitoa utetezi wake kuwa yeye ni kama samaki mzuri aliyetumbukizwa katika kapu la samaki walioza na kutumia lawama kitengo chake cha manunuzi na idara ya uhandisi kwamba hawana uadilifu wanakosa uzalendo katika utendaji kazi wao.

Johnson alisema kuwa Idara yake uhandisi ina mhandisi mmoja na wasaidizi wake wamekuwa hawana weledi wa kutosha na mhandisi mwenyewe utaalamu wake ni katika fani ya barabara na anasaidiwa na mafundi mchundo ambao pia hawana taaluma ya kutosha kuweza kusimamia ujenzi katika kiwango kinachotakiwa.

Aidha, Mkurugenzi huyo akionesha kutoridhishwa kwake na Kitengo cha Manunuzi cha Halmashauri hiyo alisema kuwa kitengo hicho kimekuwa kikiwasilisha makadirio makubwa ya gharama za ujenzi na ili kunusuru hali hiyo wakati mwingine analazimika kutumia makadilio ya hesabu za mafundi wa kawaida ili kufanya kazi ziende.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Zuwena Omari alisema mara kwa mara viongozi wamedhuru miradi hiyo na kutoa mapendekezo kwa ajili ya kuboresha ujenzi huo lakini mpaka jana wanatembelea mradi huo hawaoni nia ya kweli ya uongozi Wilayani Kishapu kuonesha wako makini katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha Zuwena alibaini mapungu katika taarifa ya utekelezaji wa miradi yote miwili kwani haonyeshi mchanganuo halisi wa kazi zilizotekelezwa au ambazo hazijatekelezwa na kumwezesha msomaji kutambua mapungufu au mafanikio katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Naye, Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ukenyenge, Anderson Mandia alisema ipo shida katika timu ya watumishi lakini yeye hawezi kusema ni wapi ila mapungufu yaliyopo wameishayabaini katika kamati ya fedha lakini pia katika Baraza la Madiwani.

Pamoja na utetezi kwa Mkurugenzi huyo Dk Philemon Sengati anaona ipo haja ya kuwajibika kutokana na Mkurugenzi huyo kutowasilisha taarifa ya uwepo wa watumishi ambao ni kikwazo katika utendaji kazi na kutaka viongozi Wilayani Kishapu kubadilika ili kuhakisi kasi iliyopo ya uchumi wakati katika kuwahudumia wananchi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/5223778bad81ac3b6c8908e596955aa4.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Na Anthony Ishengoma-Shinyanga.

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi