loader
Dstv Habarileo  Mobile
Msako wa FCC wanasa bidhaa bandia Kariakoo

Msako wa FCC wanasa bidhaa bandia Kariakoo

TUME ya Ushindani wa Biashara (FCC) kwa kushiriki na Jeshi la Polisi nchini imekamata bidhaa feki zikiwemo za rungu max zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 2.4 katika operesheni ya kushtukiza iliyofanyika katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Kazi hiyo ya ukamataji imefanyika baada ya kuwepo kwa taarifa ya bidhaa feki aina ya viwembe ambavyo vimeingizwa nchini na kuwekewa nembo ya ‘rungu max’ kinyume na taratibu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika mtaa wa Mchikichini mara baada ya kumaliza operesheni hiyo, Meneja Mauzo Kampuni ya Rungu, Noel Lema, ambaye alikuwa miongoni mwa walioendesha operesheni hiyo ya kukamata bidhaa feki alisema watafanya uchunguzi nchi nzima kuhakikisha wanapata bidhaa zote ambazo ni feki na zinatumia jina la kampuni hiyo.

Alisema duka walilofanya ukaguzi walibaini bidhaa feki aina ya wembe vilivyokuwa na lebo ya kampuni yao vikiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni 2.4.

“Watu wanatengeneza bidhaa feki mfano wembe wa rungu max original (halisi), ndani ina kikaratasi chekundu kimeandika rungu max maandishi mengi madogo, lakini feki haina hicho kikaratasi na pia watengenezaji hao wa bidhaa hizo bandia wamenakili nembo na rangi ya kampuni hiyo.

“Alafu wembe ‘original’ ukikunja hauvunjiki lakini huu unavunjika, mwisho wa siku watu wanatumia bidhaa feki wakipata madhara atasema ni ya kampuni ya rungu max wakati ni wajanja wajanja tu wanaingiza bidhaa bandia kwa hili sisi hatutakubali tutahakikisha sheria inafuata mkondo.” alisema.

“Bidhaa wanazotengeneza hususani za rungu max wamekopi vizuri nembo yetu na rangi tunayotumia, wembe asilia imetengenezwa kwa ubora na kudhibitishwa na TBS (Shirika la Viwango Tanzania) hizi za kwao ni hatari kwa afya ya watumiaji hivyo ni muhimu kuzikamata na kuziteketeza,” alisisitiza

Akifafanua bei ya katoni moja ya Rungu iliyothibitishwa na TBS ni Sh.590,000  huku bidhaa feki ikiuzwa Sh.350,000.

Naye mfanyabiashara wa duka la jumla lililokamatwa na bidhaa feki, Stephen Njira alisema kuwa bidhaa hizo alizokamatwa nazo amekuwa akizinunua kutoka kwa wamachinga huku nyingine akidai kuwa anaagiza.

“Bidhaa za rungu mimi nanunua kutoka kwa wamachinga lakini nyingine nimekuwa nikiagiza sehemu mbalimbali hapa nchini,” alisema

Kazi ya ukamataji wa bidhaa hizo umefanywa na maofisa wa FCC na askari polisi Kituo cha Msimbazi, hata hivyo maofisa hao wa tume hawakuweza kuzungumza na vyombo vya habari kwa madai kuwa msemaji wao aliyepaswa kuzungumza amepata dharura.

 


 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1910106facc7028cc1367388dbdb872e.JPG

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi