loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ummy azuia walimu kukaimu uongozi wa kata, vijiji, mitaa

Ummy azuia walimu kukaimu uongozi wa kata, vijiji, mitaa

WAZIRI wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu (pichani) amepiga marufuku walimu kukaimishwa nafasi za utendaji kwenye kata, vijiji na mitaa.

Ummy alitoa agizo hilo mjini Kibaha alipozungumza na sekretarieti ya mkoa wa Pwani na viongozi wa wilaya wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na makatibu tawala wa halmashauri za wilaya, lengo likiwa ni usimamizi wa utawala, ukusanyaji wa mapato na matumizi.

“Walimu waachwe wafundishe. Kama kuna upungufu wa watendaji wawatumie watumishi wengine hata maofisa maendeleo ya jamii,” alisema.

Alisema kama halmashauri ina mapato inaweza kuajiri kwa muda wakati taratibu za ajira zinaendelea lakini si kutumia walimu.

“Hata Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda aliomba watumishi wa idara ya kilimo nao wasikaimishwe kwenye maeneo yao ili kukabiliana na uhaba wa watumishi,” alisema.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alisema mkoa huo una fursa nyingi za kimaendeleo na viwanda na kwamba watahakikisha wanakabili changamoto zinazojitokeza zikiwemo za ardhi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/769ee107ad1d55bb38bf614a5a696967.jpeg

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi