loader
Dstv Habarileo  Mobile
MAMIA WAMZIKA HANS POPE

MAMIA WAMZIKA HANS POPE

MAMIA ya wakazi wa mkoa wa Iringa na wadau wa soka wamejitokeza katika makaburi ya Makanyagio mjini hapa kumsindikiza katika safari yake ya mwisho aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope.

Marehemu Hans Pope ambaye pia alikuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, alifariki dunia Septemba 10, 2021 katika Hospitali ya Agha Kan, Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Jimbo la Iringa parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo mshindo mjini hapo, Padri Idan Urungi alisema kifo ni ibada ambayo kila binadamu lazima aitumikie.

Alisema ni vizuri kumkumbuka Mungu wakati wa uhai ili kujiandaa vizuri kwa ajili ya safari ya mwisho.

Alisema marehemu Hans Poppe wakati wa uhai wake alikuwa mjasiri wa kuanzisha biashara na kutaka familia yake kuendeleza mshikamano.

“Tunamshukuru sana Hans Pope kwa ujenzi wa kanisa hili na ndio sababu ya familia kumleta marehemu kufanyiwa ibada ya mazishi hapa, kwani wanatambua mchango mkubwa aliokuwa akiutoa, tunashukuru pia kupata heshima hii ya kumfanyia ibada yake ya mwisho hapa, “alisema.

Akizungumza mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya club hiyo, Crescentius Magori alisema kuwa marehemu Hans Pope alikuwa na mchango mkubwa katika soka la Tanzania kupitia klabu mbalimbali, ikiwemo Lipuli FC ya Iringa.

Nao mashabiki wa Simba mkoani hapo walisema kuwa kifo cha Zakaria ni pigo kubwa kwa klabu ya Simba, hivyo watamuenzi kwa kufungua matawi mengi katika wilaya zote za Iringa.

Mungu ailaze roho ya Hans Pope mahali pema peponi, Amina.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/86912240c808aacfc2c3c4208da61c99.jpeg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Iringa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi