loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dk Kijaji avionya vyombo vya habari

Dk Kijaji avionya vyombo vya habari

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk Ashatu Kijaji amesema hatovumilia vyombo vya habari vitakavyotangaza na kuchapisha taarifa zenye lengo la kulichafua Taifa na kuwapa taharuki Watanzania.

Dk Kijaji ametoa kauli hiyo leo akiwa jijini Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo ya Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Suluhu kumteua na kumpa dhamana ya kuongoza Wizara hiyo.

"Wanahabari lazima tuchuje nini Watanzania wanataka kusikia, kile unachokiandika na kukitangaza kwenye chombo chako kiwe na maslahi mapana ya Taifa hili, kwa hili niseme sitokuwa na uvumilivu” alisema Dk Kijaji.

Alisema vyombo vya habari vinapaswa kufahamu taarifa zipi zinatakiwa kwa jamii na zisizotakiwa ili kuepuka taharuki katika jamiii.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d75665624bf780a634167f7471f47765.jpg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi