loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali yatoa taadhari mlipuko wa ugonjwa Uti wa Mgongo,

Serikali yatoa taadhari mlipuko wa ugonjwa Uti wa Mgongo,

SERIKALI imetaadharisha kuhusu  mlipuko wa ugonjwa wa  uti wa mgongo na kutaka Mikoa yote kuchukua taadhari hasa Mikoa mitano inayopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo mpaka sasa umeripotiwa kuuwa watu 129.

Taarifa ya Mganga Mkuu wa serikali, Dk Aifelo Sichwale, imeelekeza Mikoa yote hususani mikoa inayopakana au iliyo karibu na nchi ya Kongo DRC  ikiwemo Kigoma, Kagera, Rukwa, Katavi, na Songwe kuchukua hatua mbalimbali za taadhari, ikiwemo kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huo na utoaji taarifa kupitia mfumo wa utoaji taarifa za magonjwa ya mlipuko.

Amesema kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO),  Kanda ya Afrika kupitia mtandao kuwa kumejitokeza mlipuko wa homa ya uti wa mgongo katika nchi za Kongo DRC Jimbo la Tshopo. Kwa mujibu wa WHO watu 261 wameripotiwa kuugua na 129 kufariki.

“Hivyo ni vyema kuendelea kuchukua taadhari kwani  magonjwa hayana mipaka hususani mikoa inayopakana na DRC,” amesema  Sichwale.

Bakteria wa Uti wa Mgongo:

Amesema ugonjwa huo  wa mlipuko  wa uti  wa mgongo husababishwa na vimelewa aina ya bakteria wanaojulikana kama Neisseria meningitides.

Uambukizwa kwa hewa:

“ Vimelea vya ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au kukaa na mtu mwenye maambukizi.”

Amesema ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo huchukua siku mbili hadi 10 tangu kuambukizwa na kuanza kuonesha dalili.

Dalili za Homa ya Uti wa Mgongo:

Dalili Kuu ya ugonjwa huo ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma, kutapika, kuogopa mwanga, kuchanganyikiwa na shingo kukakamaa.

“Ugonjwa huo unaweza kusababisha madhara makubwa kwenye ubongo, kupotea kwa usikivu au ulemavu mwingine wa kudumu  na hata kupoteza maisha. Hivyo taadhari zinapaswa kuchukuliwa.” alisisitiza Sichwale

Kinga:

Amesema ili kuzuia maambukzi wananchi wanapaswa kuepuka mikusanyiko ya watu wengi hasa wakati wa mlipuko, makazi yazingatie mzunguko mzuri wa hewa. wananchi wanashauri kutoa taarifa mapema endapo wataona mtu yeyote mwenye dalili zilizotajwa ili hatua stahiki za kudhibiti zichukuliwe mapema.

Kuongeza nguvu ya ufuatiliaji katika mipaka hususani kwa wageni wanaoingia nchi kutoka DRC

Kuimarisha ufuatiliaji wa wagonjwa katika ngazi ya jamii hususani maeneo ya mipakani ili kutambua mapema mgonjwa yoyote anayeweza kujitokeza katika maeneo yetu, kuwandaa watoa huduma na vituo vya huduma kukabiliana na ugonjwa huu endeapo utajitokeza.

Amesema Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huo nchini DRC  na kuchukua hatua ili kuzuia na kujiandaa kukabiliana na tishio la ugonjwa huo endapo utajitokeza nchini.

“Hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi bali wanapaswa kuendelea kuzingatia kanuni za afya muda wote.” amesisitiza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/32e87b9189390d2a61727f4e71cea6a8.jpg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi