loader
Dstv Habarileo  Mobile
Muongozo wa  wasafiri namba 8 kuanza Septemba 19

Muongozo wa wasafiri namba 8 kuanza Septemba 19

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar kupitia wizara zenye dhamana ya Afya zimekubaliana kwa pamoja kuanza kutumika kwa mwongonzo wa wasafiri namba nane kuanzia   Septemba 19.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa serikali, Dk Aifelo Sichwale, ambapo alisema mwongozo huo utazingatia upimaji afya wasafiri wanaoingia nchini na upimaji Corona kwa kutumia kipimo cha haraka cha Covid 19 Rapid Antigen Test (C19RAT) kwa baadhi ya wasafiri wanaotoka katika nchi zenye maambukizi makubwa kulingana na mwenendo wa ugonjwa  kwenye nchi wanazotoka.

Alisema katika kuhakikisha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko yanayosambaa kwa kasi duniani, serikali ilitoa mwongozo wa wasafari namba saba  Mei 14, 2021.

Alisema kutokana na tathmini ya hali ya maambukizi ya Corona duniani na mahitaji ya upimajji wa ugonjwa huo nchini, serikali imehusisha mwongozo namba saba na kutoa toleo namba nane.

Alisema kutokuhitajika kwa cheti za RT – PCR wala kipimo cha C19RAT kwa watoto chini ya miaka mitano, wafanyakazi wa ndani ya ndege na abiria wanaounganisha safari wakati  madereva wa magari ya mizigo wote watapima kipimo cha haraka bila malipo wanapoingia nchini.

Aidha alisema abiria wanaoingia nchini kupitia usafiri wa nchi kavu watawajibika kuwasilisha cheti halali cha kuthibitisha kuwa hawana maambukizi ya Covid 19

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6d1567adf09a64d27030501ad54be970.jpg

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi