loader
Dstv Habarileo  Mobile
WHO YASISITIZA USALAMA HUDUMA ZA AFYA

WHO YASISITIZA USALAMA HUDUMA ZA AFYA

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limezitaka serikali na wadau wengine wa afya kupaza sauti kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa wagonjwa na uwepo wa huduma yenye hadhi na salama ya uzazi.

Aidha, limesema wakati huu wa janga la Covid-19, baadhi ya watu wamejizuia kutafuta huduma kwenye vituo vya afya kwa hofu ya kuambukizwa ugonjwa huo ama maradhi mengine, jambo ambalo shirika hilo limetaka mifumo ya huduma ya afya ijenge uaminifu kwa jamii na kuwekeza zaidi katika uzuiaji wa maambukizi.

Mkurugenzi wa WHO, Kanda ya Afrika, Dk Matshidiso Moeti, alitoa ujumbe huo jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Wagonjwa Duniani ambayo huadhimishwa kila Septemba 17.

Akizungumzia watu wanaohofia kuambukizwa Covid-19 kwenye vituo vya afya, Dk Moeti alisema: “Ili kupambana na uhitaji huu, mifumo ya huduma ya afya inapaswa kujenga uaminifu kwa jamii na kuwekeza zaidi katika uzuiaji wa maambukizi.”

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ef2ba13be1343779177a0ea6addb4148.png

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi