loader
Dstv Habarileo  Mobile
WIZARA YA AFYA ACHENI SINEMA

WIZARA YA AFYA ACHENI SINEMA

WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetakiwa  kuacha sinema za maonesho kwa kutoa maelekezo na ahadi zisizotoa matokeo yanayopimika na kuonekana kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashuri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka  mkoani Mtwara.

"Naitaka wizara ya afya kueleza kama walimdanganya Makamu wa Rais wa  Tanzania  Dk Philip Mpango, alipofika kuweka jiwe la msingi mapema mwezi Oktoba katika ujenzi wa hospital  ya kanda Mtwara inayogharimu takribani bilioni 15, ambapo walimwambia kuwa  itakuwa imeanza kutoa huduma lakini ajabu mpaka leo hakuna dalili hizo." amesema na kuongeza

"Sasa ni vizuri wabadilike waanze kuwa watendaji badala ya kuwa wapiga maneno matupu...pamoja na kasi nzuri ya ujenzi inayofanywa na mkandarasi ambaye ni shirika la Nyumba la Taifa, wizara  hiyo  imekuwa kikwazo kikubwa katika kuhakikisha hospitali hiyi inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi," amesema

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f9063e9d8125756bb1e25f8f17ca28a1.jpg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi