loader
Dstv Habarileo  Mobile
Bilioni 2.48 kujenga Chuo Buhigwe, Majaliwa aweka jiwe la msingi

Bilioni 2.48 kujenga Chuo Buhigwe, Majaliwa aweka jiwe la msingi

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma kinachojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 2.48.​

​Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la Msingi Majaliwa, amesema serikali imejizatiti katika kuhakikisha watanzania wanapata ujuzi utakaowawezesha kufanya shughuli za kiuchumi kwa weledi na kwamba katika kufanikisha mpango huo, Serikali imefanya uamuzi wa kuhakikisha inajenga chuo cha ufundi stadi katika kila wilaya nchini ili kuwezesha wananchi kupata mafunzo hayo katika maeneo waliyopo​.

​"Mkakati wetu kama serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na ujuzi unaomwezesha kutenda kazi kwenye eneo analoweza kusimamia na hatimaye kukuza uchumi wa mtu mmoja moja na taifa kwa ujumla" amesema​

​Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga, amesema ujenzi wa chuo hicho ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuwasogezea wananchi huduma muhimu za mafunzo ya ufundi stadi kwa kuhakikisha kunakuwa na chuo cha Ufundi Stadi katika kila wilaya nchini.​

​Aidha, Kipanga ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya elimu na hasa mafunzo ya ufundi stadi na kuahidi kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itasimamia ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyuo vya VETA vya wilaya ili kuhakikisha inakamilika kwa ubora na wakati.​

​Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa Chuo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Dk Pancras Bujulu, amesema Chuo hicho ni kati ya vyuo 29 vya Wilaya vinavyojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa ESPJ (Education and Skills for Productive Jobs).​

​Dk Bujulu amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2021 na kuwa kikikamilika kitatoa mafunzo katika fani za ushonaji na ubunifu wa mavazi, uhazili na mafunzo ya TEHAMA, uashi, umeme wa majumbani, ufundi magari pamoja na Uchomeleaji na uungaji vyuma na kitakuwa na uwezo wa kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa wanafunzi 240 pamoja na mafunzo ya muda mfupi kwa wanafunzi zaidi ya 960 kwa mwaka.​

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d0e6e2bf84158b179479f0cfb23c8520.jpg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi