loader
Dstv Habarileo  Mobile
Machinga Mwanza kuelimishwa kabla ya kuhamishwa

Machinga Mwanza kuelimishwa kabla ya kuhamishwa

HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza imepanga kuwatambua wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga kuanzia kesho kwa kuwapatia elimu kabla ya kuwapeleka maeneo yaliyotengwa ili kuendesha shughuli zao.

Hayo yamebainishwa jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, ambaye alisema utambuzi huo utaanza kesho Septemba 20 hadi 26, kwa kuwapiga picha katika maeneo wanayofanyia kazi zao sasa na kujaza fomu maalumu ya utambuzi.

Alisema maeneo watakayotolewa wafanyabiashara hao ni kandokando mwa barabara, mbele ya maduka ya wafanyabiashara na maeneo yaliyozibwa kwa kujengwa vibanda katikati ya jiji.

Makilagi alisema kuwa halmashauri ya jiji inakadiria kuwa na wamachinga 10,000 hadi 15,000, hivyo kazi ya utambuzi itaendeshwa kwa njia ya maelewano na kwamba itawashirikisha viongozi wa umoja wao ili kuondoa migongano pande zote.

Alisema wameunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kubaini maeneo ya kupangwa wafanyabiashara hao ambapo alitaja kuwa ni katika masoko ya Milongo watakapopangwa wafanyabiashara 170, Mbugani 650, Igogo 300 na Mchafukuoga 3,000.

Maeneo mengine ni Mkuyuni 200, Tambuka reli, Nyegezi 1,000, eneo la mbao Nyegezi na katika maeneo mengine ambayo timu hiyo inaendelea kuyabaini kwa ajili ya kuwezesha wafanyabiashara hao kufanyia shughuli zao hizo.

Alisema halmashauri hiyo inaendelea kushirikiana na mamlaka zingine kuwezesha maeneo watakayopangiwa kuwa na miundombinu yote muhimu kama maji, usafiri, vyoo na umeme.

Makilagi alisema kazi rasmi ya kuwaondoa machinga katika maeneo wasiyotakiwa itaanza Septemba 27 na kukamilika Oktoba 10 na hivyo kuliwezesha jiji kuwa na mpangilio mzuri.

Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Donata Gapi aliunga mkono wafanyabiashara kadhaa kupelekwa katika uwanja uliopo katika kata hiyo ya Mchafukuoga na kupongeza zoezi zima akisema litaondoa usumbufu unaojitokeza katikati mwa Jiji na kuhatarisha usalama wa watu.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Isamilo, Charles Nyamasiriri, alisema hatua ya kuwapanga upya machinga ni mwafaka kwani itawawezesha wafanyabiashara ambao kwa muda mrefu wameshindwa kufanya shughuli zao vizuri sasa kufanya vyema zaid

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/ac0754b6899a59806466c322d9f7c72d.jpg

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi