loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chelsea kamili, Son hatihati leo

Chelsea kamili, Son hatihati leo

Ligi Kuu England leo inaendelea katika viwanja tofauti, lakini kubwa zaidi ni mchezo unaokutanisha mahasimu wawili wa jiji la London, ‘London Derby’ kati ya Chelsea na Tottenham Spurs, mchezo utakaopigwa saa 12:30 jioni.

Kuelekea mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Totteham, wenyeji watamkosa beki wao Japhet Tanganga na kiuno Erick Dier, Lo Celso na Sanchez, huku kukiwa na tetesi kuwa huenda Heung Son naye asicheze kutokana na majeruhi.

Kwa upande wa Chelsea wataendelea kumkosa Mmarekani,Christian Pulisic, lakini wengine wote wako fiti kwa ajili ya mchezo huo.

Michezo mingine itakayopigwa leo ni West Ham United wakuwa nyumbani kuiarika Manchester United, mchezo utakaopigwa Uwanja wa London kuanzia saa 10:00 Alasiri.

Leicester City ikiwa ugenini dhidi ya Brighton itamkosa, Ayonze Perez, James Justin na Mfaransa , Wesley Fofana. Kwa upande wa wenyeji wao watawakosa, Tariq Lampatey, Adam Webster, Pascal Gross na Mholanzi, Jurgen Locadia ambao ni majeruhi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/9766a6255c89cb2473cdeb06933cbd41.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi