loader
Dstv Habarileo  Mobile
Msigwa ataka bidhaa ‘Made in Tanzania’

Msigwa ataka bidhaa ‘Made in Tanzania’

Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kuzitambulisha bidhaa hizo kwa jina la Tanzania pindi zinaposafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya matumizi.

Rai hiyo ametoa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma, ambapo pia aliruhusu maswali kutoka kwa waandishi hao na wananchi kwa njia ya simu.

Akijibu swali la mmoja wa waandishi hao, lililohoji mkakati wa Serikali kuziwekea nembo bidhaa za ndani zinazotumika nje ya nchi ili kusudi nchi hizo zitambue kuwa bidhaa hizo zimetengenezwa Tanzania.

Msigwa alisema “Serikali imechukua hatua kadhaa, kuwasimamia wazalishaji kuzitambulisha bidhaa kwa jina la nchi yetu, nitoe wito kwa wazalishaji wote bidhaa zitambulisheni kuwa zinatoka Tanzania.

Alisema katika kutekeleza hilo, kwanza Serikali imepanga kuwasimamia wazalishaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na kuziboresha.

Alisema kupitia maonyesho mbalimbali ikiwemo Sabasaba, wazalishaji wanapaswa kutumia fursa hizo kwa ajili ya kuzitambulisha bidhaa hizo zikiwa na na nembo zinazoonyesha kuwa zimetengenezwa Tanzanai.

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi