loader
Dstv Habarileo  Mobile
Majaliwa mgeni rasmi uwezeshaji wanawake

Majaliwa mgeni rasmi uwezeshaji wanawake

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la uwezeshaji wanawake kiuchumi lililopangwa kufanyika Jijini Dodoma Oktoba mwaka huu.

Kongamano hilo lina lengo la kuwakutanisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng'i Issa alisema kongamano hilo la taifa limepangwa kufanyika Oktoba 4 Jijini Dodoma.

Alisema wamejipanga na maandalizi ya kongamano hilo yanaendelea vizuri huku akiwataka wananchi kujitokeza kushiriki.

"Maandalizi yanaendelea vizuri  tunaomba wananchi mkae mkao wa kongamano kwa sababu baraza limefanya maandalizi ya kutosha,"alisema Issa.

Alisema taasisi zote za serikali na zisizo za serikali zinapaswa kushiriki katika kongamano la sita la uwezeshaji kiuchumi.

Naye, Mwenyekiti wa kongamano hilo, Suleiman Malela alisema maandalizi yanaendelea vizuri, hivyo washiriki wanapaswa kujiandaa ili kuja kuona namna ya uwezeshaji kiuchumi inavyofanyika.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1cf39abd2a98ecb3b811f2957a3139af.png

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi