loader
Dstv Habarileo  Mobile
Takwimu zaibeba Simba

Takwimu zaibeba Simba

MIAMBA ya soka nchini Simba ipo katika mazingira mazuri ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya tatu kutokana na uchanga wa wapinzani wao, Jwaneng Galaxy ya Botswana ambao wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Simba itaanza kampeni yake katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Galaxy jijini Gaborone, Botswana kati ya Oktoba 15 na 17, mwaka huu kabla ya kurudiana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam wiki moja baadae.

Wekundu wa Msimbazi wamekuwa tishio barani Afrika katika miaka mitatu ya karibuni wakiwa wamefanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili mwaka 2019 ikiwa chini ya Patrick Aussems na mwaka huu wakiwa na kocha, Didier Gomes.

Wapinzani wao Jwaneng iliyoanzishwa mwaka 2015, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano hayo na imeingia hatua ya kwanza baada ya kuiondoa Diplomates FC ya Afrika ya Kati kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 nyumbani na baadae kupoteza 1-0 ugenini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema hivi sasa nguvu kubwa wameiweka katika mchezo ujao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambao utachezwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salam.

“Mipango yetu iko katika mchezo ujao wa Ngao ya Jamii, lakini pia baada ya Ngao ya Jamii Simba itacheza michezo miwili ya Ligi Kuu dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji ndipo tutacheza mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Kamwaga.

Galaxy ilianzishwa mwaka 2015 baada ya kuungana kwa klabu mbili, Jwaneng Comets na Debswana Youngsters.

Galaxy ilipanda daraja na kucheza Ligi Kuu ya Botswana kwa mara ya kwanza mwaka 2015 baada ya kushinda michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Kusini, huku ikibakisha mchezo mmoja kabla ligi haijamalizika.

Timu hiyo kwa mara ya kwanza ilishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2018 na kutolewa katika raundi ya kwanza na CD Costa do Sol ya Msumbiji.

Timu itakayopenya hatua hiyo ya 32 bora, itafuzu kwa hatua ya makundi na kama itatolewa, itaangukia katika makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/527f990260f71de8bca7b6364c3f93fc.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi