loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga akili yote Ngao ya Jamii

Yanga akili yote Ngao ya Jamii

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Rivers United ya Nigeria, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi amekubali matokeo na kusema nguvu zao sasa wanazielekeza kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba na Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza Septemba 29.

Yanga iliondolewa kwenye michuano hiyo kwa matokeo ya jumla ya mabao 2-0, baada ya kuruhusu bao moja katika kila mchezo waliyocheza nyumbani na ugenini.

Akizungumza mara baada ya timu hiyo kurejea nchini jana kutoka Nigeria, Nabi alisema zipo sababu ambazo zimechangia kikosi chake kutofanya vizuri, lakini haoni sababu ya kuziongelea kwani wameshatolewa hivyo cha msingi kwao ni kufikiria yanayowakabili mbele.

Alisema sasa wanarejea nyumbani wakiwa kamili wakilenga kuanza kwa ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi ijayo katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Tumekuwa na changamoto nyingi, zaidi maandalizi yetu hayakuwa mazuri kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu. Tumewakosa baadhi ya wachezaji wetu kutokana na vibali vyao kuchelewa, lakini tusahau yote na tujielekeze zaidi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na ligi ambayo inatukabili,” alisema Nabi.

Kocha huyo alisema kuelekea mchezo huo watazitumia siku zilizobaki kurekebisha mapungufu machache ambayo ameyaona kwenye mechi mbili walizocheza na Rivers United, lakini ana amini wapo imara na wamejipanga kuhakikisha wanashinda.

Alisema pamoja na kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi ya Mabingwa Afrika, ameridhishwa kwa asilimia kubwa na kiwango ambacho kimeoneshwa na wachezaji wake ndio sababu ya kuwa na matumaini ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba.

Alisema kurejea kwa wachezaji kama Djuma Shabani, Fiston Mayele na kiungo Khalid Aucho kutazidi kukiimarisha kikosi chake na kuonesha ubora ambao watu walitamani kuushuhudia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/db227812d93c76536ff10178bb5fb7db.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi