loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga yaichapa DTB 3-1

Yanga yaichapa DTB 3-1

TIMU ya Yanga imeichapa DTB FC kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Avic Town, Kigamboni, Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huo ambao Yanga waliutumia kama maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, mabao ya washindi yalifungwa na Fiston Mayele, David Bryson na Athumani Yusuph, huku bao pekee la DTB inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza likifungwa na Chunga Said.

Yanga juzi iliondolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Rivers United ya Nigeria kwa jumla ya mabao 2-0 na Jumamosi inatarajia kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo wa Jumamosi wa watani hao wa jadi, tambo tayari zimeanza kwa pande zote, huku kila timu ikitamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022.

Simba ndio mwenyeji wa mchezo huo na ndio timu iliyotwaa mara nyingi Ngao ya Hisani mara tisa na Yanga imetwaa mara tano.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/a897fbfcc7b1ecaceb19bfb3d45dc723.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Na Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi