loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wakutwa na vipande 16 vya meno ya tembo

Wakutwa na vipande 16 vya meno ya tembo

WATU wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufi ji kwa tuhuma za kukutwa na vipande 16 vya meno ya tembo ambavyo thamani yake haijafahamika.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mkuranga, Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Rufiji, Protas Mutayoba, alisema watuhumiwa hao, mwanaume na mwanamke walikamatwa Septemba 22, mwaka huu.

“Tuliwakamata watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa wakiwa na nyara zinazodhaniwa kuwa ni meno ya tembo vipande 16 vyenye uzito wa kilogramu 25,” alisema.

Alisema walikamatwa katika maeneo ya UtungeKisemvule wilayani Mkuranga. Mwanaume ana umri wa miaka 40 na mwanamke ana umri wa miaka 21. Mutayoba alisema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zitachukuliwa

foto
Mwandishi: John Gagarini, Mkuranga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi