loader
Mradi kunufaisha vijiji maskini 249

Mradi kunufaisha vijiji maskini 249

WANANCHI wanaoishi vijijini watanufaika na mradi wa zaidi ya Dola za Marekani milioni sita, ili kuanza biashara ndogondogo na shughuli za kuongeza mapato.

Mradi wa Kuendeleza Ushirikiano na Raia (ACE), ulioanzishwa na Serikali ya Rwanda, Japan na Benki ya Dunia (WB) unakadiriwa kunufaisha watu 76,000 ambao nusu ni wanawake kutoka kwa kaya 17,750.

Angalau vijiji maskini 249 vitanufaika na mradi huo kupitia misaada midogo.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Taasisi za Tawala za Mitaa (LODA), Claudine Nyinawagaga, alisema mradi huo pia utasaidia kufundisha maofisa wa serikali namna ya kushirikisha raia katika mipango ya maendeleo ya mitaa.

"Utaimarisha majukwaa yetu ya ushiriki na raia katika ngazi ya mitaa, kujenga uwezo wa mamlaka za mitaa na kitaifa kuongoza mipango ya maendeleo katika ngazi ya vijiji inayohusisha kuwapa nguvu wananchi wote," alisema.

Mradi huo utatekelezwa na taasisi ya Spark Microgrants kwa kushirikiana na serikali za mitaa katika wilaya za Burera, Gakenke, Gicumbi na Huye.

Meneja wa Benki ya Dunia nchini hapa, Rolande Pryce, alisema ushiriki wa raia ni muhimu katika kuimarisha maisha endelevu ya vijijini nchini hapa na kuwa, zaidi ya kaya 70 katika kila kijiji lengwa watafaidika na kujenga uwezo kwa vikundi vya kuweka akiba.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/37cfe84572af4b32f371d2917f9a8c0f.jpg

MGANDA Jacob Kiplimo amevunja rekodi ya dunia katika ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi