loader
Wakimbizi 538 Kambi ya Gihembe wahamishwa

Wakimbizi 538 Kambi ya Gihembe wahamishwa

SERIKALI imewahamisha wakimbizi 538 kutoka Kambi ya Wakimbizi ya Gihembe huko Gicumbi ambalo ni eneo lenye hatari kutokana na kuwepo kwa maporomoko ya ardhi wakati wa mvua.

Wakimbizi hao kutoka familia 139 wamehamishiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Mahama wilayani Kirehe, ambayo maofisa walisema ni salama kwa maisha yao.

Meneja wa Kambi ya Gihembe, Goreth Murebwayire, alisema hatua hiyo inalenga kulinda ustawi wa wakimbizi na kuhifadhi mazingira.

"Tunaingia msimu wa mvua ambao unaweza kuweka wakimbizi katika hatari zaidi," alisema.

Ingawa hakujawahi kutokea tukio lolote la wakimbizi kupoteza maisha, kumekuwa na majeraha yanayotokana na watu kuanguka kwenye mitaro na korongo hali inayozidi kuweka maisha ya wakimbizi hatarini.

Zamani, Kambi ya Wakimbizi ya Gihembe ilikuwa na wakimbizi 12,314. Mapema mwaka huu, wakimbizi 2,392 walihamishiwa katika Kambi ya Mahama na 9,922 wanatarajiwa kuhamishwa ifikapo Desemba kabla ya kufungwa rasmi kwa Kambi ya Gihembe.

Naibu Mwakilishi wa  Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNCHR) nchini hapa, Boubacar Bamba, alisema: "Hii ni hatua nzuri sana kwa sababu kambi imekumbwa na janga la mazingira na mabonde mengi yaliibuka wakati wa  mvua kubwa katika eneo hili na kuweka maisha ya wakimbizi hatarini."

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b745afd0cff09776f15d377f4611b8f8.jpg

MGANDA Jacob Kiplimo amevunja rekodi ya dunia katika ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi