loader
Dstv Habarileo  Mobile
Lulu: Sikufikiria kuolewa  na mtu mwenye watoto

Lulu: Sikufikiria kuolewa na mtu mwenye watoto

MWIGIZAJI wa filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu, amesema katika maisha yake hakuwahi kufikiria kama ataolewa na mwanaume ambaye tayari ana watoto aliozaa na mwanamke mwingine.

Kupitia ukurasa wake wa Istagram, Lulu alisema: "Sikutamani kabisa kuzaa na mwanaume ambaye tayari ana mtoto. Nilikuwa na ndoto ya kuolewa na mwanaume tutakayeanzisha familia pamoja, sio mume mwenye mtoto nje ya ndoa kama dini inavyosema."

Hata hivyo, aliendelea kusema kwamba alikuja kugundua kuwa binadamu hajakamilika, wakati mwingine sio hadi awe kilema ndio aonekane hajakamilika.

"Kuna mambo mengine yanaweza kusimama kama kilema."

Lulu ambaye ameolewa na Majizo, tayari mumewe huyo ana mtoto aliyezaa na Hamisa Mobeto, hivyo kwa sasa Lulu analea watoto wote wawili.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/a875df2ecf40102b12fbc8758e2dc3c9.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi