loader
Messi aanza kutupia PSG

Messi aanza kutupia PSG

Mshambuliaji mpya wa PSG, Lionel Messi amefunga bao lake la kwanza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City, mchezo uliopigwa Uwanja wa Pac Des Princess nchini Ufaransa.

Messi amefunga bao hilo dakika ya 74 na kufanya mchezo huo kuisha kwa PSG kushinda mabao 2-0 mchezo wa kundi A wa ligi hiyo.

Bao hilo linakuwa la kwanza kwa Muagentina huyo tangu alipojiunga na matajiri hao wa Jiji la Paris Agoust 10,2021 akitoke Barcelona, baada ya kucheza michezo miwili  ya Ligi Kuu Ufaransa maarufu Ligue 1.

Bao lingine katika mchezo huo lilifungwa na Issa Gueye dakika ya nane ya mchezo huo.

Baada ya ushindi huo, PSG inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne, ikifuatiwa na Brugge KV wenye pointi nne wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya PSG.

Manchester City wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi tatu na RB Leipzig anaburuza mkia akiwa hana pointi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/81c521b72dd22ede7330c6552801c3a8.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: PARIS, Ufaransa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi