loader
Dstv Habarileo  Mobile
Sababu za Mo Dewji kusepa Simba

Sababu za Mo Dewji kusepa Simba

Kupitia mitandao yetu ya kijamii tuliripoti kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba  Mohamed Dewji amejiuzulu katika nafasi hiyo leo Septemba 29,2021 na badala yake Dewji amemteuwa aliyekuwa Makamu wake, Salim Abdallah kuchukua nafasi hiyo.

Kupitia video fupi zilizochapishwa kwenye ukurasa wake wa Twitter, Dewji amesema amefikia hatua hiyo baada ya makubaliano yaliyofanyika katika mkutano na wanachama wa bodi ya timu hiyo Septemba 21, 2021.

Aidha, mwekezaji huyo wa Simba amesema kuwa hatua hiyo imetokana na kusafiri mara kwa mara na hivyo kukosa nafasi ya kujadili mambo muhimu kwa wakati na kuongezea kuwa Salim Abdallah maarufu ‘Try Again’ atasaidia kuiongoza timu hiyo.

Mwezi Mei, mwaka jana Dewji alikubali kuwekeza Simba kwa asilimia 49 ambazo sawa na Sh bilioni 20 za hisa kulingana na maelekezo ya Serikali katika mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo kuwa kampuni.

Baada ya sintofahamu ya muda mrefu kuhusu fedha hizo, Julai 30, 2021 mwekezaji huyo alikabidhi kitita cha Sh bilioni 20 za uwekezaji ndani ya kabu hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa mfanyabiashara huyo kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo, ikumbukwe Januari 13, 2020 alitangaza kuondoka kutokana na matokeo mabaya ya Ligi ya Mabingwa na kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa mchezo wa fainali ya Mapinduzi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/06a95f7013e8afe3690843e79556042a.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi