loader
Xhaka nje miezi mitatu

Xhaka nje miezi mitatu

Kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka atakuwa nje ya Uwanja kwa miezi mitatu, baada ya kupata majeraha katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham uliopigwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Emirates.

Xhaka aliondolewa dakika ya 82 baada ya kugongana kwa bahati mbaya na kiungo wa Tottenham, Lucas Moura na nafasi yake kuchukuliwa na Sambi Lukonga. Aliumia goti la mguu wa kulia. Kocha wake Mikel Arteta amesema kiungo huyo haitaji upasuaji.

Baada ya kiungo huyo kuumia, Arsenal sasa italazimika kuwatumia, Ainsley Maitland-Niles au Martin Odegaard kwa kushirikiana naThomas Partey katika eneo la kiungo.

Kiungo huyo raia wa Switzerland atakosa pia michezo ya timu ya Taifa na atarejea uwanjani mwakani katika mwendelezo wa michezo mbalimbali.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b3e308e7619d73f41f962dcfee427d09.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi