loader
Dstv Habarileo  Mobile
NBC yadhamini Ligi Kuu Bara

NBC yadhamini Ligi Kuu Bara

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesaini mkataba wa miaka mitatu wa udhamini wa Ligi Kuu Bara na Benki ya  NBC kwa msimu wa 2021-22 ambayo tayari inaendelea NBC watatoa Sh bilioni 2.5 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Mkataba huo umesainiwa leo Oktoba 6, 2021 jijini Dar es Salaam na Rais wa TFF, Wallace Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema sehemu kubwa ya fedha hiyo itapelekwa kwenye klabu za ligi ili kuwawezesha kwenye suala la usafiri na utawala.

"Wakati udhamini wa kwanza unaingia, madhumuni makubwa yalikuwa ni katika usafiri, TFF haijabadili kitu sehemu kubwa ya fedha hii itaenda kwenye vilabu kusaidia usafiri," amesema Karia.

Aidha, Mkurugenzi wa NBC, Theobald Sabi amejipa imani kuwa mkataba huo utaendeleza ubora wa Ligi Kuu na kuongeza idadi ya wafuatiliaji katika michezo mbalimbali .

"Tuna imani kuwa mkataba huu utainua ubora wa ligi, lakini pia utaongeza chachu ya watu kufuatilia michezo katika mechi mbalimbali,," amesema Sabi.

Benki hiyo imedhamini ligi hiyo baada ya kampuni ya simu ya Vodacom kujitoa kudhamini Ligi Kuu Bara Juni 8,2121.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/912ce2aa9e2a1e642cd074509399be75.jpeg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi