loader
Dstv Habarileo  Mobile
Taifa Stars wapewa somo kuiua Benin

Taifa Stars wapewa somo kuiua Benin

SAA chache zijazo, timu yetu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’,  itakuwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kuvaana na Benin, hatua hiyo inawaamsha nyota wa zamani wa soka nchini wakiwapa darasa wenzao wa sasa nini wafanye ili washinde leo.


Golikipa wa zamani wa Taifa Stars, Muharami Mohammed, amesema anaamini Taifa Stars itafanya vizuri kinachotakiwa ni wachezaji kujiamini na hilo likifanikiwa ni rahisi kutekeleza majukumu yao.


Kauli kama hiyo imezungumzwa pia na kiungo wa zamani wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kariakoo Lindi, Mukura Victory ya Rwanda na Mlandege ya Zanzibar, Ngawina Ngawina, aliyesema wanachotakiwa ni kupunguza makosa ambayo yanaweza kuwagharimu.


“Nina imani kubwa na kikosi, vijana wahakikishe wanapata mabao ya mapema, ili kuwavunja nguvu wenyeji, tutumie vyema fursa ya kucheza mbele ya mashabiki wetu,” alisema Abubakar Mtiro, nyota wa zamani wa Yanga, Kagera Sugar na Taifa Stars.


Mchezo huo wa Kundi J kuwania kufuzu Kombe la Dunia  mwaka 2022 nchini Qatar, unatarajiwa kuanza saa 10 alasiri leo, ambapo Taifa Stars inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne, sawa na Benin, isipokuwa Taifa Stars ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/13a1be9ec68958bb80066e5a2e55e045.jpeg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi