loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rashford atunukiwa Udaktrari

Rashford atunukiwa Udaktrari

NYOTA wa timu ya Manchester United, Marcus Rashford ametunukiwa udaktari wa heshima na Chuo Kikuu cha Manchester kutokana na harakati zake zinazopinga ubaguzi, umasikini na njaa kwa watoto.

Rashford 23, ameweka rekodi ya kuwa kijana mwenye umri mdogo kutunukiwa udaktari huku harakati zake zikiwa zinakubalika na viongozi wengi akiwemo aliyekuwa Rais wa Marekani, Barrack Obama.

Akizungumza mara baada ya kutunukiwa udaktari, Rashford alitumia nafasi hiyo kueleza jinsi anavyopambana kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza kuhakikisha wanawapatia chakula watoto wenye mazingira magumu.

"Mamilioni ya familia hapa Uingereza yalipoteza mwelekeo wa maisha na upatikanaji  wa chakula, juhudi zimeonekana leo watato masikini wakisogea kwenda hatua nyingine, kwa sababu hiyo leo ni siku ya furaha kwangu," amesema Dk Rashford.

Awali Rashford alipaswa kutunukiwa cheo hicho mwezi Julai mwaka jana, ila kutokana na tatizo la virusi vya corona, hafla hiyo ilisitishwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a3d1f7384483d869c33a796619b160da.jpeg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi