loader
Neymar kuachana na Brazil

Neymar kuachana na Brazil

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe la Dunia lijalo litakalofanyika mwaka 2022 litakuwa la mwisho kwake kuitumikia timu yake ya Taifa.

Kauli ya Neymar 29 ilitolewa kwenye jarida la Neymar & The Line Of Kings, lililotengenezwa na mtandao wa michezo wa DAZN na kuchapishwa kwenye mtandao wake wa Twitter.

"Nadhani litakuwa kombe langu la mwisho," Neymar alisema. " sijui kama nitaweza kuwa sawa kiakili, kuvumilia soka."

"Nitafanya kila linalowezekana kufika huko. Nitafanya kila niwezalo kushinda kombe nikiwa na nchi na hapo nitakuwa nimetimiza ndoto yangu, kubwa tangu ujana wangu." Aliongeza Neymar.

Neymar alicheza katika sare ya 0-0 dhidi ya Colombia Jumapili kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia, hata hivyo inasemekana alicheza chini ya kiwango hali iliyofanya baadhi ya mashabiki kuanza kumtolea maneno machafu.

Kocha wa Brazil, Adenor Leonardo Bacchi ‘Tite’ aliulizwa juu ya uchezaji wa chini ya kiwango wa Neymar, ambao ulijumuisha pasi 17 zilizopotea.

"Ni mchezaji wa kipekee kwa sababu anacheza kwa kipekee, anafanya kipekee na sio kawaida," alisema. "Ni mchezaji maalum, tunajua, pia alikuwa amekabwa na watu zaidi ya wawili,” alisema Tite.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/687b4a249557aa657a3c4d5e9a8a687e.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: SAO PAULO, Brazil

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi