loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tari Kibaha wapongezwa  kuboresha kilimo cha miwa

Tari Kibaha wapongezwa kuboresha kilimo cha miwa

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI), Kituo cha Kibaha imepongezwa kutokana na kuwashirikisha maofisa ugani wa Wilaya ya Kilosa na kuwapatia utaalamu wa namna bora ya kuimarisha kilimo cha miwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Kidodi (Amcos) wilayani humo, Onesmo Mwakyambo alisema maofisa ugani katika wilaya hiyo wanaoshughulika na utoaji wa elimu kwa wakulima kuhusu zao la miwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuwaelimisha namna bora ya kuongeza tija katika kilimo hicho.

Mwakyambo alisema maofisa ugani katika wilaya hiyo wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya kitaalamu na wataalamu wa Tari Kibaha na hivyo kutumia maarifa hayo kuwaelimisha wakulima, hatua iliyochangia kuboresha uzalishaji wa zao hilo.

“Tuna uhakika ndani ya miaka mitano ijayo uzalishaji wa miwa utaongezeka sana, wataalamu wetu wamekuwa na mchango mkubwa katika kutupatia maarifa na ndiyo maana hata vijana wengi kwa sasa wamevutiwa na kilimo cha miwa. Ni jukumu la serikali sasa kusimamia ukuaji wa viwanda vya sukari ili miwa isipotee,” alisema.

Ofisa Ugani wa Kijiji cha Kielezo, Kata ya Ruhemba, Joyce Edward alisema: “Sisi kama wataalamu tunapata faraja kubwa kuona wakulima wetu wanayafanyia kazi maelekezo tunayowapa na hivyo kuwa na mashamba bora ambapo kwa sasa tunawahamasisha vijana kutumia muda wao mwingi katika uzalishaji wa miwa ili kuondokana na umaskini,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/4f15c33d22e5de46acae249110042f5e.jpg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi