loader
Dstv Habarileo  Mobile
Miradi yenye utata kufikishwa kwa Rais Samia

Miradi yenye utata kufikishwa kwa Rais Samia

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, na Walemavu, Jenista Mhagama amesema baada ya mwenge kuzimwa taarifa ya miradi iliyoshindwa kuzinduliwa itafikishwa mbele ya Rais Samia kwa ajili ya uwajibishaji.

Mhagama amesema hayo  wilayani Chato mkoani Geita katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza miradi yote iliyobainika kuwa na mapungufu taarifa zake zitafanyiwa kazi.

Amesema itakapobainika kuna ubadhilifu wa fedha za miradi ama imejengwa chini ya kiwango wahusika watasubiria maamuzi yatakayotolewa na Rais juu ya ukamilishwaji wa miradi hiyo.

“Viongozi ndani ya serikali yetu wakishindwa kutekeleza majukumu yao, maagizo na miongozo ya serikali na hasa katika kuzingatia matumizi sahihi ya raslimali fedha ni lazima wachukuliwe hatua,” amesisitiza.

Mwenge wa Uhuru ulipokelewa mkoani geita oktoba 9 mwaka huu na unatarijiwa kuzimwa oktoba 14 wilyani chato na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f6ec1a6e470281c559f4d36efa897dde.jpg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Yohana Shida, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi