loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kata ya Kawekemo Mwanza yatengewa Tsh milioni 315/- miradi mbalimbali

Kata ya Kawekemo Mwanza yatengewa Tsh milioni 315/- miradi mbalimbali

Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dk Angeline amesema Kata ya Kawekemo iliyopo Wilaya ya Ilemela imetengewa Tsh milioni 315 kwajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dk Mabula amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya daraja la Msumbiji darajani, ambapo amesema kuwa katika fedha hizo kuna Tsh milioni 178 zilizotengwa kwajili ya ujenzi wa barabara za kiwango cha lami.

Alisema pia Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela imetenga Tsh milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili kwa shule za msingi ni Pasiansi na Kilimani.

Dk Mabula amesema ofisi yake imefanikiwa kupeleka matofali 1800 kwajili ya ujenzi wa Zahanati ya kawekamo na kukamilika zahanati hiyo inahitaji matofali 5000.

Diwani wa kata ya Kawekamo Omary Juma amesemaa anamuomba mbunge wa jimbo hilo kuwasaidia katika ukamilishaji wa zahanati ya Kawekamo ambapo inahitaji shilingi milioni 50 kwajili ya kufunika jengo la zahanati.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/05c35a82f928498e0f56ef4efc282e23.jpg

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ...

foto
Mwandishi: Na Alexander Sanga,Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi