loader
MBINU 10 ZA KUZUIA USALITI KWENYE MAPENZI (SPOTILEO)

MBINU 10 ZA KUZUIA USALITI KWENYE MAPENZI (SPOTILEO)

USALITI au udanganyifu katika mapenzi hauepukiki na ni wimbo uliozoeleka kwa wapendanao. 
Inaaminika kwamba karibu kila mshiriki wa uhusiano, hata awe mwaminifu kwa kiasi gani, wakati fulani amedanganya angalau mara moja.

Kwa nini? Mshauri John Horward anasema ni kutokana na asili ya mapenzi yenyewe kuwa ni kitu cha siri na kinachoshawishi udadisi hivyo kufanya wengi kuvutiwa kujaribu kwingine ili kutafuta ladha mpya (labda!).

Wakati mwingine, anasema, mioyo hutamani tu kupata changamoto mpya ili kuwepo na ulinganifu wa mapenzi iwe katika kutafuta kilicho bora au kucheza tu (playing!).

Na tatizo hili lipo zaidi kwa wanaume kwa mujibu wa Howard huku walio katika ndoa au mahusiano ya kudumu wakitajwa kuongoza katika usaliti na udanganyifu.

Kwa mujibu wa takwimu takribani asilimia 50  ya ndoa au mahusiano ya kimapenzi huvunjika kwa ajili ya usaliti.
Anasema ingawa kuvunjika kwa uhusiano kwaweza kusababishwa na sababu tofauti, lakini usaliti na 'kuibiana' ndio sababu kubwa na inayoumiza sana wapendanao.

"Usipovunjika (uhusiano au ndoa), hudhoofika kutokana na ile dhana ya usaliti kutofutika kirahisi mioyoni," anasema.
Na anaweka msisitizo ya kwamba zaidi ya nusu ya wapenzi hudanganyana huku akielezea pia umuhimu wa tatizo hilo katika baadhi ya nyakati katika mapenzi.

Anashtua kwa kugusia kwamba wakati mwingine 'kutoka nje' husaidia kuupa afya uhusiano. Kwa nini? Wakati ambapo wanandoa au wapenzi huchokana na kutotilia mkazo misingi muhimu ya ujenzi wa mshikamano miongoni mwao au kupoteza mawasiliano kuhusu mahitaji na matamanio muhimu, uwepo wa uhusiano mbadala unaweza kurahisisha wakarudi kwenye mstari.

Usaliti wakati mwingine unaweza kuwa njia mojawapo ya kuimarisha uhusiano unaoyumba kwani ili kuzuia wizi kila mmoja atataka kuboresha mazingira ya utimilifu wa kila hitaji la mwenza wake ndani ya nyumba.

"Lakini kwa ujumla wake usaliti si mzuri na unazalisha maumivu makali mapenzini," anasisitiza John Howard.
Ni muhimu kubaini vyanzo vya usaliti katika mapenzi namna ya kuzuia 'ajali' hiyo isikutokee katika uhusiano wako.
Hii ni kwa sababu usaliti una madhara makubwa katika uhusiano na maisha kwa ujumla kwani kama ni ndoa, ikivunjika huathiri ustawi wa watoto, ndugu na jamaaa pia.


1. MAKUBALIANO

Dr. Stan Tatkin katika mchango wake kuhusiana na hili anaona njia sahihi ya  kufanya ni kuwepo kwa makubaliano ya wazi baina ya wapendanao dhidi ya udanganyifu na usaliti.

“Wakati mwingine ni dhana tu ya usaliti na si kila kinachodhaniwa hutokea,” anasema.
Makubaliano yaweke wazi mipaka ya kila mmoja. Taaria zipi za kuchangia (zinazowavutia wote) na wakati wa kujulishana mambo muhimu ya uhusiano na kupeana uzoefu.

Kuwepo na mazungumzo juu ya mambo yanayoweza kupelekea usaliti au maana ya usaliti katika mapenzi.
Kwa mfano, mwanaume anaweza kudhani kwamba si tatizo yeye kwenda muziki na rafiki wa jinsia tofauti wakacheza dansi na hata kupigana busu hadharani ilhali kwa mwenzi wake huo ni usaliti wa hali ya juu.


2. MAPENZI MATAMU

Kinga bora ya kuzuia usaliti katika mapenzi ni kuwa na uhusiano imara kama mwamba. Mahitaji yote ya kimwili na nafsi yakitimizwa ndani ya nyumba hakuna haja ya mtu kutoka nje. 

Tathmini ni kwa ubora kiasi gani unamtimizia mwanaume wako mahitaji yake na anavyofanya yeye kwako. Boresha maeneo yenye mapungufu na kwa uwazi mjulishane mahitaji ya kila mmoja ili kujenga uhusiano mtamu na kuachana na usaliti kwani hakuna jipya huko nje!

3. PAMOJA KAMA KUMBIKUMBI

Kwa kuwa mnapendana ni lazima yapo mambo mengi ya pamoja mtakuwa mnafanana na mengi kati ya hayo yanapaswa kufanyika pamoja kama kumbikumbi.

Fanya mambo yanayoweza kuwaendeleza pamoja kwani mabadiliko mengi hutokana na umri hivyo usikubali kuachwa nyuma.
Ukaribu katika maisha ya kawaida ya kila siku na mapenzi huongeza upendo na uwazi na kuminya fursa ya mmojawapo kusaliti penzi kirahisi.

4. MJUE MWENZI WAKO

Inachukuliwa kwa urahisi lakini sivyo. Kumjua mwenzi wako kuliko yeyote. Mwanaume wako ana siri na mawazo binafsi ambayo ni vigumu kuyatambua kirahisi. Unapaswa kumhakikishia usalama ili afunguke kwako kila kitu upate kumjua vizuri. Kivipi? Tengeneza mazingira ya kumjua mpenzi wako kwa undani kuliko mwingine ili ujue ni wakati gani amehitaji kufaniwa nini!

Tambua mambo yake ambayo hata mama yake au ndugu na marafiki hawajui. Ufahamu huo utakuongezea thamani ya tofauti kwake ambayo hatathubutu kuilinganisha na yeyote nje.

5. ACHA WIVU, KUWA BORA 

Unapobaini kuwa mwenzi wako ameanza kupepesa macho nje, hasira na wivu si suluhisho bali huzidi kumkimbiza.
Wivu ni lazima katika mapenzi lakini jaribu kutumia vipaji vyako vyote kumfanya akuone bora, akupende na kukuthamini na si kumlazimisha.

Sababu chanya za kuwa pamoja naye ni sawa na gundi ya kuwaunganisha pamoja inayoziba mianya ya 'wezi' kuingilia uhusiano wenu. Maoni 0713 214721
Itaendelea

foto
Mwandishi: Na George John

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi