loader
Dstv Habarileo  Mobile
NEMC YASHIRIKI MAONESHO YA UTALII YA AFRIKA  MASHARIKI

NEMC YASHIRIKI MAONESHO YA UTALII YA AFRIKA MASHARIKI

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira linashiriki katika Maonesho ya kwanza ya Utalii ya nchi za Afrika Mashariki yaliyozinduliwa mwishoni mwa Oktoba 9, 2021 na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki yanalenga katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii nchini, bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa katika sekta ya utalii.

Katika maonyesho hayo NEMC inatoa elimu ya uhifadhi wa mazingira ikiwemo suala zima la umuhimu wa wawekezaji kufanya tathmini ya Athari kwa mazingira (TAM) kabla ya kuanzisha miradi katika sekta ya utalii.

Pia limepokea changamoto za kimazingira kutoka maeneo mbalimbali nchini hususani katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nyeti kiikolojia, usimamizi wa taka ngumu na kelele chafuzi.

Katika maonyesho hayo ya kwanza ya utalii ya Nchi za Afrika Mashariki, kampuni mashirika na taasisi 155 yameshiriki.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/98dbe03bafb0115f38ce4daa4d8185ff.jpeg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi