loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ma-RC watakiwa kuwasilisha andiko la wajasiriamali

Ma-RC watakiwa kuwasilisha andiko la wajasiriamali

OFISI ya Rais-TAMISEMI imewaelekeza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanapeleka andiko mahususi la maeneo watakayoboreshea wajasiriamali kabla ya Oktoba 20, mwaka huu.

 

Aidha, viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri wametakiwa kuepuka safari zisizo za lazima zinazohusu kutoka nje ya mkoa isipokuwa kwa kibali katika kipindi cha utekelezaji wa miradi hii.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu ameagiza hilo jana alipoelezea Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya Covid-19 katika Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

 

Ummy alisema kabla ya Oktoba 20, mwaka huu, wakuu wa mikoa na wa wilaya wahakikishe wanawasilisha Tamisemi andiko mahususi la maeneo yatakayoboreshwa na kubainisha kiasi cha fedha kinachotumika kulingana malengo yaliyokusudiwa.

 

Alisema jumla ya Sh bilioni tano zimepangwa kutumika katika mpango wa kuboresha mazingira ya kufanyia shughuli za wajasiriamali ambako uchambuzi umeonesha kuwa maeneo yenye wafanyabiashara wadogowadogo ni majiji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Tanga, Mwanza na Manispaa za Ubungo, Kinondoni, Temeke na Morogoro.

 

Alisema azima ya serikali imepanga kuwezesha wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo kwa kuboresha mazingira ya kufanyia shughuli zao wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

 

Aidha, ametoa maelekezo mahsusi kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuunda Kamati ya Mkoa ya uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi husika na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu Tamisemi kila wiki mbili.

 

Pia kuhakikisha kila halmashauri inaunda Kamati ya Halmashauri ya uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi na utekelezaji wa miradi unaanza ndani ya wiki mbili baada ya fedha kupokelewa.

 

Ummy alisema halmashauri zitakazotaka kufanya mabadiliko ya utekelezaji wa mradi, maombi yawasilishwe kwa maandishi kwa Katibu Mkuu Ofisi Rais - Tamisemi ndani ya wiki moja baada ya kupokea fedha hizo.

 

Amesisitiza utekelezaji wa miradi uzingatie thamani ya fedha na ubora wa miradi na watoa huduma wa vifaa, mafundi watangaziwe kazi zilizopo kupitia tovuti za mikoa, halmashauri pamoja na mbao za matangazo katika ofisi za umma.

 

Pia amezitaka halmashauri zinaelekezwa kufanya manunuzi ya pamoja ili kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi na mameya na wenyeviti wa halmashauri pamoja na madiwani wote kupitia kamati zao kuhakisha wanasimamia miradi hii kwa kushirikiana na watendaji wa halmashauri.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0216363acda101c0ec31438250d04d69.jpeg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi