loader
Dstv Habarileo  Mobile
Jarida lampongeza Samia vita ya corona

Jarida lampongeza Samia vita ya corona

JARIDA maarufu Afrika la Forbes limemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kama kiongozi wa kwanza mwanamke anayeliongoza kwa uimara na huruma taifa lake katika kuliponya na janga la ugonjwa wa Uviko-19, kuwezesha ukuaji wa uchumi na kuandaa vizazi vijavyo kwa fursa kubwa zaidi.

 

Forbes lilibainisha hayo katika toleo lake la Oktoba/Novemba mwaka huu.

 

Jarida hilo lilibainisha kuwa baada ya kuapishwa kuwa Rais Samia, mpango wake wa haraka ulikuwa kushughulikia suala la Covid-19 kwa kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kuunda Kamati ya Wataalamu kwa ajili ya kuchunguza namna Tanzania inavyoweza kukabiliana na ugonjwa huo.

 

“Ndani ya wiki tatu tangu aingie madarakani, Rais Samia alifanikiwa kuunda kamati ya wataalamu ili kumshauri kuhusu hali ya Covid-19 nchini na hatua muhimu za kuchukua ili kuwaweka salama Watanzania,” ilisema Forbes.

 

Kutokana na janga hilo la Covid-19, Forbes imebainisha kuwa katika mwaka 2020 uchumi ulishuka huku ajira kwenye sekta nyingi zikipotea na wengine wakihofu kuwa uchumi ungeendelea kuathirika katika kipindi cha mwaka huu na mwakani na kusababisha changamoto kwa maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.

 

Kwa mujibu wa Forbes, Rais Samia alieleza kwa uwazi kuwa utawala wake utaendelea na mipango ya maendelo iliyopo ikiwemo Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025 ambayo itasaidia kupatikana tena kwa unafuu wa muda mrefu kutokana na janga hilo.

 

“Hivi karibuni alianzisha mpango wa kufufua uchumi akitolea mfano diplomasia ya uchumi, utoaji motisha kwa miradi ya kimkakati, kupambana na rushwa na ufisadi, kuondoa urasimu katika utoaji wa vibali vya kazi na kuidhinishwa kwa miradi ya uwekezaji, ambapo yote hayo yanalenga kuchochea ukuaji wa uchumi walau kwa asilimia nane kwa mwaka,” ilisema Forbes.

 

Jarida hilo lilisema Rais Samia aliwahi kusema kuwa ukuaji wa uchumi ulishuka kutoka wastani wa asilimia 6.6 hadi asilimia 4.7 mwaka jana, hivyo unahitajika uwekezaji mkubwa ili kukuza uchumi na kuzitaka mamlaka za Tanzania zinazohusika na kodi, uhamiaji na leseni za biashara kutekeleza sera zinazowafaa wawekezaji wa kigeni ili kuvutia uwekezaji na kuchochea taifa katika ukuaji mkubwa wa uchumi.

 

Forbes lilisema mipango mingine ya Rais Samia ilikuwa kuiunganisha nchi, kulinda uhuru wa kimsingi na kukuza sauti za kidemokrasia pamoja na kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungwa hapo awali.

 

Pia lilitaja mpango mwingine wa maendeleo ambao ni sehemu ya ajenda ya Samia ni kuifanyia kazi sera ya hali ya hewa na kuongeza kuwa Rais Samia ni ishara ya mabadiliko makubwa kwa Tanzania.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/03c720672a610c2df20416ef0c09e808.jpeg

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi