loader
Dstv Habarileo  Mobile
Z’bar kuimarisha ushirikiano na Comoro, Namibia

Z’bar kuimarisha ushirikiano na Comoro, Namibia

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema Zanzibar iko tayari kuendeleza uhusiano na ushirikiano Muungano wa Visiwa vya Comoro ukiwemo wa kibiashara.

 

Alisema hayo Ikulu mjini Unguja jana alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Muungano wa visiwa hivyo nchini Tanzania, Dk Ahamada El Badoi Mohamed Fakih.

 

Dk Mwinyi alisema uhusiano huo ni kichocheo kwa wafanyabiashara wa Zanzibar na Comoro kuimarisha sekta ya biashara, na kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na wananchi wataendeleza na kudumisha uhusiano na ushirikiano huo sambamba na kuendeleza sekta za uchumi.

 

Balozi Fakih alimueleza Dk Mwinyi umuhimu wa kurudisha utamaduni wa wafanyabiashara wa Comoro kwenda kufanya biashara Zanzibar na wa Zanzibar kwenda Comoro kwa ajili hiyo.

 

Wakati huo huo, Dk Mwinyi jana alikutana na kuzungumza na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Lebbius Tangeni. Balozi huyo alikwenda Ikulu kujitambulisha.

 

Katika mazungumzo walieleza umuhimu wa kuendelezaji ushirikiano katika sekta za kiuchumi vikiwemo viwanda, biashara, uwekezaji na uhusiano ya miji na manispaa za Zanzibar na Namibia.

 

Balozi Tangeni alisema ameazimia kukutana na uongozi wa ngazi za mikoa wa Zanzibar, viongozi wa Manispaa na Jiji la Zanzibar, na uongozi wa Mamlaka ya Ukuzaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA).

 

Dk Mwinyi alimueleza Balozi huyo dira ya serikali anayoiongoza ya Uchumi wa Bluu na akasisitiza kwamba Namibia ina nafasi nzuri katika kushirikiana na Zanzibar.

 

Mapema jana Dk Mwinyi alikutana na kuzungumza na Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Dk Eliezer Felishi. Dk Feleshi alikwenda Ikulu Zanzibar kujitambulisha.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e8ac93a149f3e63a71804820faa86b9e.jpeg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi