loader
Dstv Habarileo  Mobile
Warioba: Wakemeeni wanaoleta ukabila

Warioba: Wakemeeni wanaoleta ukabila

WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba amesema ni wajibu wa viongozi pamoja na wananchi kukemea wote wanaoleta masuala ya ukabila, udini, ukanda pamoja na uvyama ili taifa lirudi kwenye misingi aliyoianzisha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

 

Jaji Warioba alisema hayo wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana.

 

Alisema Nyerere aliishi bila ubaguzi hata maadui zake walikubali alikuwa mwadilifu kwani aliitumikia nchi hakuiibia.

 

“Mwalimu hakupenda sana kutengeneza sanamu hukusikia mahali popote panaitwa Jina lake, hakutaka kuitwa mheshimiwa alisema wote ni ndugu.

 

“Alibaki ni mtu muadilifu kwa nchi yake. Sasa mambo yake aliyoyaishi kuna umuhimu zaidi ya kuyazingatia. Hivi sasa ukabila unaanza kuzungumzwa sana, udini unaanza kuzungumzwa sana, ukanda unaanza kuzungumzwa sana, u vyama pia, ile misingi ambayo ilijenga umoja na amani tunaanza kuiiingilia,” alisema Jaji Warioba.

 

Alisema chuo hicho cha Mwalimu Nyerere ndio chimbuko la viongozi waliokuwepo waadilifu, waaminifu na wamejitolea kutumikia nchi yao.

 

“Tunaweza kujifunza zaidi kwa matendo yake Mwalimu, tunazungumzia amani, ilijengwa haikuja hivi hivi,” alisema na kuongeza kuwa Mwalimu alikuwa na nia ya wazi kujenga taifa lenye umoja pamoja na taifa lenye amani.

 

Alisema Mwalimu Nyerere alitaka itumike Lugha ya Kiswahili kwenye mawasiliano ya hadhara kwa wakati ule haikuwa rahisi, lakini kwa sasa ndiyo lugha iliyounganisha Watanzania.

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara, Philip Mangula alisema Mwalimu Nyerere aliamini katika kujenga umoja kupitia vikao kwani hata mawazo aliyokuwa nayo aliyafikisha kwenye vikao kabla hajachukua hatua yoyote.

 

Alimnukuu kuwa katika kitabu chake cha 'Tumetoka wapi, tunaenda wapi’ kinaonesha umoja na mshikamano ndio unasaidia kupambana na dhuluma.

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisema anamfahamu Mwalimu kwa kuwa alifanya kazi naye kwa miaka 20, na kwamba aliamini katika kutambua utu wake na wa wengine kwa kuheshimu, kutoa uhuru pamoja na kutoa nafasi ya kusema kwa wengine.

 

“Mwalimu alikuwa Mwafrika sana. Alijenga taifa kwa usawa na kujitegemea. Alijenga umoja na mshikamano, tulijenga taifa la kujitegemea sio kuwa ombaomba. Ukipewa uongozi uhakikishe nchi zetu hazituletei zogo,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d40e6b561339b816212b7a8495e43619.jpeg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi