loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mganga Mkuu wa Serikali ahimiza tafiti za magonjwa

Mganga Mkuu wa Serikali ahimiza tafiti za magonjwa

MGANGA Mkuu wa Serikali, Dk Aifello Sichalwe amesema tafiti sahihi ni silaha muhimu kukabili changamoto za magonjwa yakiwamo ya mlipuko.

Alisema hayo wakati akifungua kongamano la nane la afya Tanzania linalofanyika jijini Dodoma.

"Wizara inasisitiza zaidi umuhimu wa tafiti za magonjwa hasa nyakati hizi za milipuko ya magonjwa kama Covid 19, mafanikio yetu kama taifa katika kutatua changamoto za kiafya yanategemea sana kazi za utafiti wa kitabibu," alisema.

Dk Sichwale alitoa rai kwa watafiti katika sekta ya afya kujikita katika kufanya tafiti za kutafuta ufumbuzi wa changamoto za afya zinazokabili jamii.

Aidha, alihimiza jamii kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na virusi vya corona ikiwamo kupata chanjo kwani ni salama na inaokoa maisha ya watu, inapunguza mnyororo wa kuenea kwa ugonjwa, kupunguza ukali wa virusi na kuwalinda wengine ili maisha ya wananchi yaendelee kama awali.

 

“Serikali imeongeza dozi za chanjo ya corona ili kuongeza kasi ya mapambano ya ugonjwa wa Covid-19 na kuwasisitiza wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa lugha nyepesi ambayo wataielewa,” alisema.

Dk Sichwale alisema serikali imefanya kazi kubwa kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga miundombinu ya afya na kununua vifa tiba.

Akizungumzia kongamano hilo, Dk Sichwale alisema mkutano huo wenye kaulimbiu ya 'Asiachwe mtu nyuma', inahitaji mipango sahihi na madhubuti katika sekta zote hususani ya sekta ya afya.

Awali, Rais wa Kongamano la Afya Tanzania, Dk Omary Chillo alisema mkutano huo umelenga kuboresha afya kupitia uwezeshaji na kutoa taarifa za afya za kuaminika na kuiwezesha jamii kushiriki katika majadiliano yenye kuleta tija katika kuboresha sekta ya afya.

"Pia tunakusudia kushirikiana na wadau wa afya kuunga juhudi za serikali hasa kwenye ugonjwa wa Covid-19, kuboresha utafiti katika sekta za afya na tangu tuanze machapisho ya kitafiti 500 yamejadiliwa na mwaka huu machapisho 103 ya kisayansi yatachapishwa," alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/93491b8fbf93268310c6458722ba6b20.jpeg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi